Na Masanja Mabula – Pemba
MKUU
wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib amewaomba wazazi na walezi
katika Shehia ya Makangale kukubaliana na maamuzi atakayochukua dhidi
ya vijana wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu katika shehia hiyo.
Amesema
kila mzazi anapaswa kuyaunga mkono maamuzi hayo kwani lengo ni
kurejesha maadili kwa vijana ambayo yanazidi kuporomoka kutokana na
waliowengi kujiunga na vikundi vya ulevi.
Akizungumza
na wananchi wa shehia hiyo , kwenye kikao cha kusikiliza kero za jamii ,
Salama amewaonya wazazi ambao wataingilia maamuzi yake na kusema
atawajumuisha kwenye orodha ya wahalifu.
‘Ninayo
orodha ya vijana wanajihusisha na vitendo vya ulevi , naomba sana
wazazi msingilie maamuzi yangu , na atakaye ingilia nitakuwa sahaani
moja naye ’’alisisitiza.
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya ameelezea kusikitishwa na baadhi ya wananchi wa
shehia hiyo kufungua klabu za kuanza kuuza pombe bila ya kuwa na kibali
na kuutaka uongozi wa shehia kuzifunga .
Mapema
mwakilishi wa wananchi haaaaao Rashid Habib amesema maadili kwa vijana
yanazidi kuporomoka , kwani baadhi ya vijana wanajiingiza katika vitendo
vya unywaji wa pombe .
Amesema
hali hiyo imesababishwa na ongezeko la klabu za pombe mabazo zimefikia
nne , na hivyo kuwafanya vijana kujiingiza kwenye vikundi viovu .
‘Hili
pia limesababisha ongezeko la vitendo vya wizi wa mazao pamoja na
mifugo , hivyo tunaomba nguvu kutoka serikalini tumechoka kwani tumeanza
kunyemelewa na umaskini’’ alisema.
Naye
Rehema Makame amesema uwepo wa vijana wanaojihusisha na ulevi unawanya
wavunjike moyo kuendelea na shughuli za kilimo cha zao la mwani .
Amesema
baadhi ya vijana wanashindwa kuwakemea kwa hofu ya kupokea kipigo kwani
huwa wamevuta bangi na wakati mwengine kunywa pombe hivyo chochote
wanaweza kukifaanya .
No comments :
Post a Comment