Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice
Tanzania Bw. Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari wakati
alipowatangaza washindi Wakazi wawili wa jiji la Dar
es Salaam ambao ni wachumba Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard
walioibuka washindi wa shindano la Harusi ya Ndoto Yako lililokuwa
likiendeshwa na chaneli ya Maisha Magic Bongo Dstv chaneli 160.
Wachumba
Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard walioibuka washindi wa shindano la
Harusi ya Ndoto Yako lililokuwa likiendeshwa na chaneli ya Maisha Magic
Bongo Dstv chaneli 160 wakizungumza machache mara baada ya kutambulishwa
mbele ya waandishi wa habari leo..
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akizungumza katika hafla hiyo huku Wachumba Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard wakimsikiliza kwa furaha.
Meneja Masoko wa Multchoice
Tanzania Alfa Mria na akizungumza jambo na Fisa Masoko na Uhusiano Bi.
Shumbana Walwa wakati wa hafla hiyo.
Bi Shumbana Walwa Afisa Masoko na Uhusiano Multchoice Tanzania akizungumza jambo wanaomsikiliza ni wachumba Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande kulia akiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakifuatilia mambo kadhaa katika hafla hiyo.
……………………………………………………………………………………………………….
- Ni ya washindi wa shindano la ‘Harusi ya Ndoto Yako’
Wakazi wawili wa jiji la Dar es
Salaam ambao ni wachumba Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard wameibuka
washindi wa shindano la Harusi ya Ndoto Yako lililokuwa likiendeshwa na
chaneli ya Maisha Magic Bongo Dstv chaneli 160.
Wapenzi hao wameshinda zawadi ya
ufadhili wa harusi yao ya kifahari itakayofanyika jijini Dar Es Salaam
mwishoni mwa mwezi April mwaka huu. Pamoja na kushinda Harusi ya Ndoto
Yao, wawili hawa pia watapewa zawadi ya fungate kwa hisani ya hoteli ya
kitalii ya Voyager Beach iliyopo jijini Mombasa nchini Kenya.
Washindi hao walitangazwa jana
katika kilele cha siku ya wapendanao katika hafla iliyofanyika makao
makuu ya MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
washindi hao.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande amesema
channel ya Maisha Magic Bongo imeamua kuwatunuku watazamaji wake zawadi
hiyo kupitia kipindi chake maarufu cha Harusi Yetu kinachorushwa na
channel hiyo ambacho huonyesha harusi mbalimbali
Kipindi cha Harusi Yetu kilianza
kuruka mnamo Novemba 2016 ambapo msimu wa pili wa kipindi hicho ulianza
mwezi Julai mwaka 2017. Kipindi hicho hurusha harusi mbamlimbali huku
kikiangazia walikotoka wanandoa, hatua wanazopitia katika mahusiano yao
na hatimaye tukio la kufunga ndoa.
Kuanzia ilipoanza awamu ya pili
Maisha Magic Bongo ilianzisha shindano maalum lililojulikana kama Harusi
ya Ndoto Yako ambapo washiriki walikuwa wakijibu kuhusiana na kipindi
cha harusi yetu ambapo kila wiki kulikuwa na swali moja. Hadi kufikia
mwisho wa shindano mnamo mwezi Desemba mwaka jana jumla ya washiriki
1,112 walishiriki ambapo 448 waliingia kwenye mchujo wa wawali na
hatimaye kubakia wanne ambao waliitwa kwenye usaili maalum uliokuwa na
jopo la watahini saba.
Baada ya usaili huu, Solomon
mkazi wa Dar es Salaam pamoja na mchumba wake Magreth waliibuka washindi
na hivyo kupata zawadi ya kugharimiwa harusi yao itakayofanyika jijini
Dar es Salaam mnamo tarehe 28 mwezi April mwaka huu.
Akifafanua kuhusu zawadi hiyo,
Maharage alisema zawadi hiyo inamaanisha maharusi hao watarajiwa
watagharimiwa kila kitu kuanzia ukumbi, mavazi, chakula, vinywaji,
burudani, pamoja na fungate la kukata na shoka katika moja ya hoteli za
kitalii Voyager Beach Hotel katika ufukwe wa Mombasa nchini Kenya.
Wakizungumza katika hafla hiyo,
Solomon pamoja na mchumba wake Magreth wamesema wamefurahi sana kushinda
na kutuzwa ufadhili wa harusi yao. “Sote tunafahamu ni jinsi gani zoezi
la harusi linavyokuwa na patashika hususan kwenye suala la gharama.
Hivyo nafurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kushinda
katika shindano la Harusi ya Ndoto Yangu kwani sasa sisi kazi yetu ni
kufikiria tu jinsi tutakavyoendesha maisha yetu kwani suala la harusi
limekamilika” alisema Solomon, Bwana Harusi mtarajiwa.
Ameipongeza Chaneli ya Maisha
Magic Bongo kwa kubuni shindano hilo ambalo lilileta msisimko mkubwa na
kwamba anaamini kuwa channel hiyo itaendelea kuimarika kwani kwa sasa
imekuwa maarufu sana kwa kuwa ni chaneli inayowafanya watanzania
wajivunie vipaji vyao.
DStv kupitia chaneli yake mahsusi
ya maudhui ya Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele
katika kuhakikisha kuwa tasnia ya Sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya
vyanzo muhimu vya mapato kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi
wa nchi yetu.
Chanel ya Maisha Magic Bongo
ilianzishwa tarehe 1 Octoba 2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza
vipaji na Sanaa hapa Tanzania na pia kuongeza maudhui ya kitanzania kwa
wateja wa DStv. Kwa kipindi chote hiki Chaneli hii imekua kwa haraka
sana ambapo kwa sasa ni miongoni mwa Chaneli zenye watazamaji wengi
zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Chaneli hii imekuwa kitovu cha
maendeleo ya wasanii hapa nchini huku mamia ya wasanii wakipata fursa
mbalimbali kutokana na kazi zao kurushwa katika channel hii na pia
kupata mafunzo na kipato kupitia Sanaa.
Kwa upande wa tasnia ya filamu na
uigizaji, Maisha Magic Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa
filamu zinazotikisa katika soko kwa sasa ni pamoja na Tamthila ya
HUBA,ambayo ilipokelewa vizuri sana na Watanzania, pia kuna filamu na
vipindi vingine kama SARAFU, KAPUNI, MWANTUMU, HARUSI YETU, KITIMTIM
pamoja na tamthilia mpya zilizoanza kuonyeshwa hivi karibuni za SARAFU
na KAPUNI ambazo zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.
No comments :
Post a Comment