Muanzilishi
wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya
wakati (Njiti), Doris Mollel (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa
wauguzi wa zamu wa Wadi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya
Mwananyamala, sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia
Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali hiyo ikiwa ni katika
kuadhimisha siku ya kuonyeshana upendo (Valentine's Day) ambayo
huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Februari 14. Taasisi ya Doris
Mollel walishirikiana na Kampuni ya MakJuice na baadhi ya wapigapicha,
wanahabari pomoja na wadau wengine waliojitoa kufanikisha zoezi hilo,
lililofanyika jana jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Warda Walid
(Muwakilishi wa Taasisi ya DMF Zanzibar), Mariam Gerion (DMF Dar es
salaam), Mtangazaji wa Clouds TV, Shadee pamoja na baadhi ya wauguzi wa
Hospitali hiyo.
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo pamoja na vitu vingine mbalimbali.
Muwakiliwa
wa Kampuni ya MakJuice, Zahir akimkabidhi zawadi ya khanga mmoja wa
kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali
ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Muanzilishi
wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya
wakati (Njiti), Doris Mollel akizungumza jambo na mmoja wa kinamama
waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya
Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Wakinamama waliojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), wakipoza koo zao na Juice za Mak walipotembelea Hospitalini hapo.
No comments :
Post a Comment