WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali imetumia sh. bilioni 161.9 kuboresha vituo vya afya 170
nchini pamoja na kugharamia huduma ya Afya ya Mama na Mtoto kwa lengo
la kuokoa maisha yao.
Amsema Serikali itaendelea
kukarabati na kupanua miundombi
nu ya kutolea huduma pamoja na kununua
vifaa vya kisasa katika Hospitali za Mloganzila, Benjamini Mkapa, Dodoma
na Hosptali za Rufaa katika Mikoa na Kanda.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumatano, Februari 14, 2018) wakati akizindua jengo jipya la mama na
mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Amana iliyopo wilayani Ilala
jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo la ghorofa mbili limejengwa kwa ufadhili wa kundi la kampuni za AMSONS na lina thamani ya sh bilioni 1.2.
Amesema uzinduzi wa jengo hilo
unakwenda sambamba na azma ya Rais Dkt. John Magufuli za kuimarisha
sekta ya afya na kuifanya kuwa miongoni mwa sekta za kipaumbele.
Amesema lengo la Serikali ni
kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi. “Mfano,
Hospitali za Rufaa za Amana, Mwananyamala na Temeke, zimeendelea
kuhudumia wagonjwa kutoka Zahanati, Vituo vya Afya vya Serikali, binafsi
na vya dini kutoka mikoa jirani ya Pwani, Morogoro na Lindi.
Pia amesema Serikali itaendelea
kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 –
2020, kuhusu kuwapatia wananchi huduma bora za afya pamoja na kujenga
hospitali nyingine za Rufaa kwa ajili ya Kanda ya Kusini, Kati na
Magharibi.
Akizungumzia kuhusu changamoto ya
idadi ndogo ya watumishi na ukosefu wa huduma za uangalizi maalumu
(ICU) katika hospital ya Amana, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea
kufanyia kazi changamoto zote zilizopo katika sekta ya afya zikiwemo n
aza hospital hiyo.
Waziri Mkuu amesema Serikali
itaendelea kuthamini na kutambua mchango wa wadau mbalimbali pamoja na
kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa huduma za afya nchini
zinaboreshwa.
Hivyo, alitumia fursa hiyo na
kulipongeza kundi la kampuni za AMSON’s lililoamua kujenga jengo la mama
na mtoto katika hospital hiyo kwa ushawishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Bw. Paul Makonda.
Awali, Mganga Mkuu Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa – Amana, Dkt. Meshack Shimwella alisema wazazi wanaolazwa
katika hospitali hiyo kwa siku ni 180 hadi 250 na uwezo wa hospitali ni
vitanda 353, ambapo vitanda 250 vinatumika wodi ya wazazi.
Alisema idadi hiyo hailingani na
idadi ya wagonjwa, hivyo kusababisha wakati mwingine wagonjwa kulala
zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja kutokana na kasi ya ongezeko wa
wagonjwa wanaolazwa hususani wodi ya watoto na akinamama.
Dkt. Shimwella alisema
wamefanikiwa kuongeza jingo la kutolea huduma ya mama na mtoto lenye
ghorofa mbili ilililojengwa kwa ufadhili wa AMSONS lenye uwezo wa
vitanda 100, ambalo ndilo liliongeza idadi ya vitanda kutoka 253 hadi
kufikia 353.
“Kutokana kukamilika kwa jengo
hilo kwa sasa akinamama wanaonyonyesha wanalala wakiwa mmoja mmoja,
watoto wachanga wanahudumiwa katika mazingira mazuri yanayofanana na
viwango Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Bw. Makonda aliwashukuru wafadhili waliojenga jengo hilo
kwa sababu si kila mtu anayekwenda hospitali na kukuta changamoto na
akaamua kuzifanyia kazi.
Bw. Makonda alisema awali
akinamama walikuwa wanalala hadi watatu katika kitanda kimoja, hivyo
madhumuni ya ujenzi wa jego hilo ni kupunguza msongamano katika wodi ya
wazazi.
No comments :
Post a Comment