
Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi serikali kupitia wizara ya
Maji kulipa kwa wakati wakandarasi waaminifu wanaosimamia miradi ya
Maji ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu.
Mheshimiwa Aweso ameyasema hayo
Jijini Dar kwenye siku yake ya nne ya kikazi alipokuwa akikagua
maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa na Manispaa pamoja na Miradi
ya DAWASCO na DAWASA.
“Wizara ya Maji inajitahidi
kutengeneza miradi ya maji itakayomaliza tatizo la Maji kwa wananchi
hususani wananchi wenye kipato cha chini hasa vijijini, hivyo mkandarasi
atakayefanya kazi yake vizuri na kwa wakati sisi kama serikali
hatutasita kumlipa kazi yake kwa wakati”alisema Aweso
Katika ziara yake hiyo, Mheshimiwa Aweso alitembela miradi ya Maji ya Hondogo, Kibamba, Kingazi A pamoja na Mburahati.
Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akiangalia bomba lililopasuka.




No comments :
Post a Comment