Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Profesa Simon Msanjila (katikati) akizungumza jambo wakati wa mkutano na
Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kulia) na Mshauri masuala ya
Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya
Canada, Jeffrey Davidson (kushoto).
Watendaji mbalimbali kutoka
Wizara ya Madini na Ubalozi wa Canada nchini Tanzania wakifuatilia
majadiliano kwenye mkutano wa Katibu Mkuu Madini na Balozi wa Canada
(hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya na kulia ni
Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy. Wengine ni
Maafisa kutoa Wizara ya Madini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Profesa Simon Msanjila (kulia) akimsikiliza Mshauri masuala ya
Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya
Canada, Jeffrey Davidson (katikati). Kushoto ni Balozi wa Canada nchini,
Ian Myles (kulia).
Mshauri masuala ya Uwajibikaji
kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey
Davidson (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (katikati). Kulia ni Balozi wa
Canada nchini, Ian Myles.
Balozi wa Canada nchini, Ian
Myles (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia). Katikati ni Mshauri masuala
ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya
Canada, Jeffrey Davidson.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Profesa Simon Msanjila (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa
mkutano na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles (katikati). Kulia
ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya
Madini, Profesa Shukrani Manya. Kutoka kushoto ni Mshauri masuala ya
Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya
Canada, Jeffrey Davidson na Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada
nchini, Anita Kundy.
……………………………………………………………………………………………………………………….
Kampuni za Madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata Sheria za nchi ili kuepuka migongano.
Wito huo umetolewa jijini Dar es
Salaam Januari 29, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa
Simon Msanjila kwenye mkutano na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles
aliyeambatana na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia
ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson.
Ujumbe huo ulimtembelea Katibu
Mkuu Msanjila kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali kwenye Sekta
ya Madini ikiwemo suala la Sheria ya Madini, masuala ya uwajibikaji kwa
jamii (CSR) yanayofanywa na kampuni mbalimbali zikiwemo za kutoka nchini
Canada na matarajio ya Serikali kwa kampuni (wawekezaji).
Profesa Msanjila alisisitiza kuwa
kampuni zinazofanya shughuli zake nchini zinalazimika kufuata taratibu
na sheria za nchi ili kujijengea mazingira rafiki ya utekelezaji wa
shughuli husika.
Alisema lengo la Serikali ni
kuhakikisha Sekta ya Madini inanufaisha Taifa kwa ujumla sambamba na
wawekezaji na alibainisha kwamba lengo hilo litafikiwa ikiwa kampuni
husika zitatekeleza wajibu wake kwa uwazi kulingana na matakwa ya
sheria.
“Kampuni zinazojihusisha na
shuguli za madini zinapaswa kufanya shughuli zake kwa usahihi na uwazi,”
alisisitiza Profesa Msanjila.
Aidha, Profesa Msanjila
alisisitiza kuwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za madini nchini,
zinapaswa kupata taarifa sahihi kutoka kwa Wataalam waliopo Serikalini
ili kupata mwelekeo sahihi wa dhamira ya Serikali.
“Kampuni zinatakiwa kupata
taarifa sahihi kutoka kwa vyanzo sahihi ili kufanya shughuli zake kwa
usahihi,” alisisitiza Profesa Msanjila.
Profesa Msanjila vilevile
alizungumzia dhamira ya Serikali ya kuhakikisha madini yanayochimbwa
nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa nje ili kukuza uchumi
wa Taifa.
“Madini yakiongezwa thamani hapa
nchini, faida ni nyingi ikiwemo ajira na pia mapato yataongezeka kwani
tutakuwa tumeelewa thamani halisi ya madini husika, kabla
hayajasafirishwa,” alisema.
Ili kufikia dhamira hiyo, Profesa
Msanjila alisema Serikali ipo kwenye mazungumzo na kampuni
zilizoonyesha nia ya kujenga viwanda vya kuyeyusha na kusafisha madini
(smelting and refining).
Mbali na hilo, Profesa Msanjila
alizungumzia suala la uwezeshaji wachimbaji wadogo wa madini ambapo
alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba wananufaika ipasavyo na
shughuli zao sambamba na mchango wao kwenye pato la Taifa kuonekana.
Alielezea jitihada mbalimbali
zinazofanywa na Serikali katika kuwawezesha wachimbaji wadogo ikiwemo
uanzishaji wa vituo vya mafunzo vya mfano (centre of excellence) ambavyo
alivitaja baadhi yake kuwa ni Kituo cha Tanga, Geita na Mtwara.
Kwa upande wake Balozi Myles
alisema ni muhimu Serikali, Wawekezaji na Jamii kwa ujumla kushirikiana
na pia kuwa na lengo la wazi la namna ya kunufaika kutokana na Sekta ya
Madini.
Naye Davidson aliahidi kuzungumza
na kampuni za Canada kuelezea matarajio ya Serikali kwao kwa namna
mbalimbali ikiwemo suala la sheria, uwajibikaji kwa jamii, mazingira na
michango mbalimbali ya kampuni kwa maendeleo ya jamii.
“Nitawakumbusha kwamba
wanawajibika si kwa wanahisa wao peke yake bali pia kwa jamii
wanapofanyia shughuli zao,” alisema Davidson.
Mkutano wa Katibu Mkuu wa Madini
na Balozi wa Canada nchini ulihudhuriwa na watendaji mbalimbali kutoka
Wizara ya Madini akiwemo Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya.
No comments :
Post a Comment