Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo
wakati wa kikao cha kupokea msaada kutoka mfuko wa fedha wa pamoja
(Global Fund) kilichofanyika jana katika Ofisi za Waziri Mkuu jijini Dar
es salaam.
Meza kuu, Ikiongozwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
(wapili) wakati wa kikao cha kupokea msaada kutoka mfuko wa fedha wa
pamoja (Global Fund), kushoto kwake ni Mwakilishi kutoka Global Fund
Tatjana Peterson, kulia kwake ni Pro. Faustine Kamuzora, wa mwisho ni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Picha ya pamoja ikionesha zoezi la kutia saini baina ya Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Fedha wa pamoja (Global Funds).
Picha ya Pamoja ya Makabidhiano ya Mkataba yaliyo sainiwa na Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Fedha wa pamoja (Global Funds).
…………………………………………………………………………………………………
Na WAMJWW. DSM
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jnsia, Wazee na Watoto imetia saini Shilingi Tilioni 1.1 na mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund) kwa ajili ya kupambana na magonjwa ya UKIMWI, MALARIA na KIFUA KIKUU.
Hayo yamebainishwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa kikao cha Makubaliano ya kusaini fedha hizo kilichofanyika jana katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, napenda kuwashukuru sana Global Funds, kwa kuendelea kushirikiana nasi katika kutatua changamoto za
rasilimali fedha katika kupambana na
UKIMWI, MALARIA na KIFUA KIKUU” alisema Mh. Ummy Mwalimu.Na WAMJWW. DSM
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jnsia, Wazee na Watoto imetia saini Shilingi Tilioni 1.1 na mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund) kwa ajili ya kupambana na magonjwa ya UKIMWI, MALARIA na KIFUA KIKUU.
Hayo yamebainishwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa kikao cha Makubaliano ya kusaini fedha hizo kilichofanyika jana katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, napenda kuwashukuru sana Global Funds, kwa kuendelea kushirikiana nasi katika kutatua changamoto za
Mh. Ummy aliendelea kusema kwamba utekelezwaji wa makubaliano ya shughuri hii utasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu huku miradi ikitekelezwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya Raisi TAMISEMI pia Mashirikayasiyo yakiserikali na Sekta Binafsi.
Pia Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha fedha hizo zilizotolewa na Mfuko wa Fedha wa pamoja kutumika kikamilifu ili kuweza kupata matokeo yaliyotarajiwa ya Asilimia 90 ya wananchi kupima UKIMWI ili kujua hali zao, Asilimia 90 ya Watanzania walio na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI waweze kutumia dawa ya kufubaza Virusi hivyo (ARV) na Asilimia 90 ya wanaotumia dawa za ARV, Virusi viwe vimefubazwa (90,90,90).
Mbali na Hayo Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa Asilimia 40 ya Watanzania wameweza kufika katika vituo na kupata tiba, huku lengo ni kuhakikisha kwamba itakapofika mwaka 2020, asilimia 70 ya wenye maambukizi ya Kifua kikuu wawe wanajulikana na kuanza kupata huduma za matibabu mara moja.
Kwa upande wa Malaria fedha hizo zitatumika katika kupunguza maambukizi ya Malaria ili kufikia Asilimia 1 ifikapo mwaka 2020.
Akiwawakilisha Makatibu Wakuu wenzake Prof Faustine Kamuzora ameahidi kusimia matumizi sahihi ya fedha zote walizopokea kutoka kwa Mfuko huo katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa ufanisi mkubwa na kwa maadili ili kufikia malengo waliyojipangia.
“Tutahakikisha kwamba fedha zote zilizopatikana zinatumika vizuri na kuhakikisha kwamba matokeo makubwa yanapatikana, Afya za Watanzania zinahimarika kwa kufanya usimamizi mzuri.” Alisema Prof Kamuzora.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Global Fund Tatjana Peterson ameahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kupambana na magonjwa ya UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu.
Nae msindika Makohozi Bw. Paskali Mbagala ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusogeza huduma ya kupima na kutibu magonjwa ya Kifua Kikuu kwa wananchi hususani wa vijijini, jambo lililosaidia kupunguza vifo vya watu wengi.
Akiwasilisha Taarifa ya Baraza la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Mwenyekiti wake Bw. Justine Bunyoka ameiomba Serikali kuendeleza ushirikiano wa karibu na Mfuko huo ili kurahisisha kufikisha Huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
No comments :
Post a Comment