Na Mwandishi Wetu,Dodoma
NAIBU Waziri wa Elimu ,Sayansi na
Teknolojia,William OleNasha,amefafanua utaratibu wa kupata cheti
mbadala/uthibitisho kwa mtu aliyepoteza cheti ambapo ameeleza kuwa
Baraza la Mitihani litafanya kazi hiyo kwa muda usiozidi siku 30.
OleNasha aliyasema hayo leo
bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mafinga
Mjini,Cosato Chumi (CCM) lililokuwa likihoji ‘’Je ni utaratibu gani
unaotumika pale mtu anapopoteza cheti ili aweze kupata cheti
kingine’’?,Je ni unapata cheti halisi au nakala? na ni taratibu gani
anatakiwa kuzifuata mtu ili ombi lake lifanyiwe kazi ifuatavyo na bila
kucheleweshwa?.
Katika majibu yake Naibu Waziri
huyo alieleza kuwa mhitimu aliyepoteza cheti hupatiwa cheti
mbadala/uthibitisho wa matokeo kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi
kuhusu upotevu wa cheti na kupata hati ya upotevu.
Pia mtu aliyepotelewa na cheti
atatakiwa kutangaza gazetini kuhusu upotevu huo kwa lengo la kuutaarifu
umma ili kusaidia kukipata na endapo cheti hakitapatikana hata baada ya
kufuata utaratibu huo ,mhitimu atajaza fomu ya ombi la cheti mbadala
/uthibitisho wa matokeo na kuiwakilisha Baraza la Mitihani.
‘’Baada ya mhitimu kujaza fomu
hiyo Baraza la Mitihani hufanya uchunguzi wa uhalali wa umiliki wa cheti
husika na kutoa huduma stahiki ,wahitimu waliofanya mtihani kuanzia
Mwaka 2008 ambao vyeti vyao vina picha hupatiwa vyeti mbadala ‘’alisema
na kuongeza kuwa
“Na waliofanya mtihani kabla ya
Mwaka 2008 hupatiwa uthibitisho wa matokeo ambao hutumwa kwa waajiri wao
au mahali pengine kwa mahitaji yaliyotolewa na mwombaji na kundi hilo
halipewi cheti mbadala’’
Alisema cheti mbadala
kinachotolewa ni cheti halisi ambacho huongezwa maandishi yanayosomeka
’DUBLICATE’ kuonyesha kuwa cheti hicho kimetolewa mara ya pili.
No comments :
Post a Comment