Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini (TPSF) Dk Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP LTD, amekipatia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake
Tanzania ( TWCC) jengo la maonyesho la IPP Ltd lililopo ndani ya viwanja
vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili
liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali.
Jengo hilo pamoja na kuendeleza
ujasiriamali litakuwa eneo la maonesho na kufunzia na Dk Mengi amesema
amelitoa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwawezesha wanawake
kiuchumi. Maamuzi ya kutoa jengo hilo yalifuatana na ombi lililotolewa
na Mwenyekiti wa TWCC Jacqueline Maleko aliyetaka jengo hilo kupewa
wanawake ili kuwaendeleza kiuchumi na kimafunzo.
Akizungumza wakati wa kufungua
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania
(Tanzania Women Chamber of Commerce-TWCC), Dk Mengi aliwataka wanawake
kuwa macho na kutumia fursa zilizopo kujiwezesha kiuchumi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini TPSF Dr. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mwakilishi wa
TRA, Rose Mahendeke (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya
Wajasiriamali Wanawake nchini TWCC, Bi. Noreen Mawalla (wa pili
kushoto), Mwenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini (TWCC),
Bi. Jaqueline Mneney Maleko (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi
wa mikutano wa Benki Kuu kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha
Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce
(TWCC) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Aliwataka wanawake kuthubutu na kuwa
wajasiri katika kuangalia na kuzitumia fursa zilizopo sasa nchini badala
ya kuzipita bila kuziona. Aidha Dk Mengi aliwataka wanawake wajiamini
na kujihakikishia kwamba wanaweza kujiletea maendeleo, wawe wanyenyekevu
katika biashara zao, na wawe na ndoto kubwa ya maendeleo huku wakianza
kidogo kidogo badala ya kusubiri mtaji mkubwa.
Katrika mkutano huo Dk Mengi alitoa
ushuhuda wa jinsi yeye alivyoanza biashara zake na kusema alitumia fursa
alizoziona kutengeneza dawa ya kung’arisha viatu baada ya kuchukua mkaa
Kariakoo na kuusaga na kuchanganya na mafuta. Alisema alitengeneza dawa
iliyoitwa ‘Sunshine’ na alivuna mapesa.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye
pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akizungumza wakati akifungua
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania –
Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa
mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema kwamba alianzia
kutengeneza kalamu ndani ya sebule kabla hajaondoka na kutumia maeneo ya
nje kutengeneza kalamu na kasha kuwa na kiwanda kikubwa. Alisema yeye
alizaliwa katika umaskini akiishi katika nyumba ya msonge pamoja na
wanyama na kuamua kuukataa umaskini. Alisema kilichomsaidia yeye ni kuwa
na macho yanayoona Fursa na kuitumia vilivyo kwa kujiamini na
kuthubutu.
Alisema Mungu aliumba kila mtu kuwa
namba Moja na ni vyema watu wote wakajiona kuwa namba moja na katika
hilo kuthubutu huku wakihakikisha kwamba wanatumia vyema teknolojia
iliyopo kwa kufanya matangazo ya biashara zao. Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC, Bi.
Noreen Mawalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania TWCC
Jacqueline Meney Maleko (hayupo pichani) kutoa neno la ukaribisho kwa
mgeni rasmi na wanachama wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
mwaka wa TWCC uliofunguliwa jana jijini Dar es Salaam.
Aliwataka kutumia simu zao
kuhakikisha kwamba wanauza na kuzitangaza bidhaa zao huku akiwataka
wakue na kuacha kuogopa kuanzisha viwanda. Pia aliwataka kuwa
wanyenyekevu katika biashara zao kwani ndio namna bora ya kuendeleza
urafiki wa kibiashara kati yao na wadau wanaohitaji huduma au bidhaa
zao.
Alisisitiza utoaji wa bidhaa bora
hata kama bidhaa hizo zimelenga kuwasaidia watu maskini na kuwataka kila
senti wanayoipata katika biashara kuhakikisha inabaki hukohuko na
isichanganywe na matumizi binafsi. Mapema akimkaribisha mgeni rasmi
kwenye mkutano huo, Mwenyekiti TWCC, Jacquiline Maleko alipendekeza
Chama chake kiwe na ushirikiano na uwakilishi mkubwa kwenye taasisi
muhimu za biashara na kuyataka makampuni binafsi nchini yawe yananunua
bidhaa za wanachama wao kabla ya kupendelea bidhaa za nje. Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline
Mneney Maleko akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dr.
Reginald Mengi kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa TWCC unaoendelea
katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Maleko pamoja na kumuomba Dk Mengi,
kuipatia TWCC jengo lililopo Sabasaba pia aliitaka TPSF (sekta Binafsi)
kuhakikisha kwamba inawazungumzia wanawake na kuwapa nafasi katika vikao
vya maamuzi. Pia alifafanua kwamba chama hicho kinataka kushirikishwa
katika baraza la biashara la kitaifa na mikoani kwa lengo la kutetea
wanawake ambao asilimia 50 ya wafanyabiashara nchini ni wao.
Maleko alisema chama hicho
kilichoundwa mwaka 2005 na kwa sasa kikiwa na majukwaa 11 pote nchini,
kimelenga kuunganisha nguvu za wanawake katika kuhakikisha wanashika
uchumi kwa kutumia fursa zilizopo za nafasi mbalimbali za wanawake
zilizowezeshwa kitaratibu, kama asilimia 5 ya mapato ya halamashauri
kusaidia makundi maalumu na asilimia 30 ya zabuni ya manunuzi ya
serikali kupewa makundi maalumu. Mkurugenzi
wa Huduma za Uanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Louis
Accaro akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa
Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of
commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es
Salaam.
Alishauri asilimia hiyo tano
kukopeshwa SACCOS yao wanawake ili waweze kukopa na kuendeshea biashara
zao, akiamini kwamba fedha hizo zikifikishwa zitawatoa wanawake
kiuchumi. Alisema kwa sasa wanawake wafanyabiashara wamekuwa
wakikabiliwa na matatizo ya mila, desturi na taratibu za kisheria na
hivyo wao ni kazi yao kuhakikisha kwamba sauti ya mwanamke inafika kila
mahali ili mazingira ya biashara yaboreshwe.
Maleko pia alisema kama serikali
inaweza kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa kwanini na wao wasipewe ruzuku
hiyo ili waweze kuinua uchumi wa taifa. Pia waliomba nafasi katika
maeneo ya Taasisi ya viwanda vidogo SIDO kutumiwa na wanawake kuanzisha
viwanda vya kusindika vyakula ambapo pia wanaweza kufundishwa na
watalamuwa SIDO wakiwa palepale. Meneja
mikopo ya wanawake na uwezeshaji wanawake wa benki ya CRDB nchini,
Rehema Shambwe akitoa salamu za benki hiyo kwa wajumbe wa TWCC wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake
Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika
ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa mwaka ulifadhiliwa na
Mamlaka ya Kodi na Mapato TRA, uilikuwa na wageni wengi wakiwemo watu wa
CRDB ambao wanampango wa kuanzisha kituo cha kusaidia wanawake katika
masuala ya biashara na ujasiriamali na Trade Mark ambao tayari
wanaushirikiano na TWCC.
Akizungumza katika mkutano huo
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga
alisema Asasi yake ipo katika hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa
miaka 5 wenye thamani ya shilingi bilioni mbili na Chama hicho, baada
wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650 kuhitimishwa. Mkataba huo wa
mwanzo ulishughulika na mafunzo kwa wajasiriamali katika nyanza zote
kuanzia uzalishaji na ufungashaji na matumizi ya hati mbalimbali
zinazogusa ujasiriamali. Mwakilishi
wa TRA ambao ndio wamefanikisha kufanyika kwa mkutano huo, Bi. Rose
Mahendeke aktioa salamu za TRA kwa wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania
– Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi
wa mikutano wa Benki kuu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga akitangaza
kuhusiana na hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wa
thamani ya shilingi bilioni mbili na TWCC, baada wa ule wa mwanzo wa
shilingi milioni 650 kuhitimishwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women
Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko
akishuhudia Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr
Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akiweka kwa
maandishi kukabidhi jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo ndani ya
viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili
liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali. Kulia ni
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha
juu na chini ni wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka
unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye
pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney
Maleko (katikati) kibali cha jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo
ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es
salaam, ili liwasaidie wanachama wake kuendeleza ujasiriamali. Kulia
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha
juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr
Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD
akisalimiana na wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano mkuu wa
mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Salaam. Mgeni
rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald
Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD katika picha ya
pamoja na wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea
katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Saalaam Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia
ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa TWCC, Bi. Noreen Mawalla.
No comments :
Post a Comment