Monday, January 29, 2018

MSEMAJI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI ATEMBELEA CHANNEL TEN

  Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja (katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtangazaji mwandamizi wa Channel Ten na Magic fm, Kibwana Dachi katika studio za Channel Ten, (kushoto) ni Damian Muheya na Nasibu Mgosso (kulia) wakiwa ni Maafisa habari wa Jeshi hilo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.

  Mwandishi wa habari na mtangazaji mwandamizi wa African Media group Ltd inayosimamia Vyombo vya utangazaji Channel ten na Magic Fm, Bw. Kibwana Dachi akifafanua jambo kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.

  Mkuu wa Kitengo cha kurusha matangazo Channel Ten, Bw. Abdallah Lugisha akitoa ufafanuzi jinsi mitambo ya kurusha matangazo inavyofanya kazi kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja akiwa ameambatana na Maafisa habari wa Jeshi hilo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.

 Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja akijibu swali kutoka kwa mtangazaji wa Magic Fm Salma Msangi katika kipindi cha Busati wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.
  (PICHA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI)

No comments :

Post a Comment