Thursday, January 25, 2018

KITUO CHA REDIO CHA TIMES FM CHATOA TUZO JKCI YA KUTHAMNI NA KUTAMBUA KAZI NZURI ILIYOFANYWA MWAKA 2017 KWA KUTOA HUDUMA BORA YA MATIBABU YA MOYO NA KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA


Picha no. 1

Mkurugenzi wa kituo cha Redio cha Times Fm Rehure Nyaulawa akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi tuzo ya kuthamni na kutambua kazi nzuri waliyoifanya kwa mwaka 2017 ya kutoa huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuokoa maisha ya watanzania. JKCI ni moja ya Taasisi za Serikali ziliyopewa tuzo na Times FM.

Picha no. 2

Mkurugenzi wa kituo cha Redio cha Times Fm Rehure Nyaulawa akimkabidhi tuzo   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi tuzo ya kuthamini na kutambua kazi nzuri waliyoifanya kwa mwaka 2017 ya kutoa huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuokoa maisha ya watanzania. JKCI ni moja ya Taasisi za Serikali ziliyopewa tuzo na Times FM.

picha no. 3

Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kituo cha Redio cha Times Fm wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa  hafla fupi ya kukabidhi tuzo ya kuthamini na kutambua kazi nzuri iliyofanywa  na JKCI  kwa mwaka 2017 ya kutoa huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuokoa maisha ya watanzania. JKCI ni moja ya Taasisi za Serikali ziliyopewa tuzo na Times FM

picha no. 4

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza wafanyakazi wa  kituo cha Redio cha Times Fm jinsi Taasisi hiyo inavyofanya kazi wakati wa   hafla fupi ya kukabidhi tuzo ya kuthamini na kutambua kazi nzuri iliyofanywa  na JKCI  kwa mwaka 2017 ya kutoa huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuokoa maisha ya watanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa kituo cha Redio cha Times Fm Rehure Nyaulawa.

Picha no. 5

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza wafanyakazi wa  kituo cha Redio cha Times Fm madhara ya ulaji vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi nyingi, uvutaji sigara na unywaji wa pombe uliopitiliza kwa afya ya moyo. Wafanyakazi wa Times FM walitembelea Taasisi kwa ajili ya kukabidhi tuzo ya kuthamini na kutambua kazi nzuri iliyofanywa  na JKCI  kwa mwaka 2017 ya kutoa huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuokoa maisha ya watanzania

Picha no. 6

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza wafanyakazi wa  kituo cha Redio cha Times Fm jinsi Taasisi hiyo inavyofanya kazi wakati wa   hafla fupi ya kukabidhi tuzo ya kuthamini na kutambua kazi nzuri iliyofanywa  na JKCI  kwa mwaka 2017 ya kutoa huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuokoa maisha ya watanzania.
Picha na JKCI

No comments :

Post a Comment