Wednesday, January 24, 2018

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGEKAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE


????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi  (kulia) wakizungumza na Mbunge  wa viti maalumu, ambaye pia ni Mjumbe  wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii,  Zainabu Mwamwindi  wakiwa wameongozana na Wajumbe Kamati hiyo  wakati walipotembelea jana Jengo la Makumbusho ya  Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya  Binadamu katika Mamlaka ya Hifadhi  ya Ngorongoro.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi  (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,    Japhet Hasunga (kushoto)  wakiwa  na Wajumbe Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii  wakati walipotembelea jana Jengo la makumbusho ya  Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya  Binadamu katika Mamlaka ya Hifadhi  ya Ngorongoro
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii , Kemilembe Luota ( wa kwanza kushoto)  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Japhet Hasunga (katikati)  pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii  Maj. Gen. Gaudence Milanzi  (wa pili kulia)  wakiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati hiyo  wakiwa kwenye ‘’View Point’ kituo ambacho hutumika kuangalia bonde la  Ngorongoro kabla ya kutelemka katika Bonde hilo jana wakati walipofanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro
????????????????????????????????????
Huyu ndiye Faru Fausta  ni  faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia.
????????????????????????????????????
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii  na Waandishi wa habari wakiji’selfie’ katika banda la Faru Fausta  ambaye ndiye  faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia wakati walipotembelea banda hilo kwa ajili ya kujionea
????????????????????????????????????
Baadhi ya Msururu wa Magari yaliyokuwa yamewbeba wjumbe wa kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara pamoja na wa Ngorongoro kwa ajili ya kutelemka kwenyeBonde la Ngorongoro.
????????????????????????????????????
Baadhi ya  wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa katika  nje ya ofisi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuanza ziara.
????????????????????????????????????
Kundi la Simba wakiwa wamepumzika walipoonekana jana wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii  ilipofanya ziara ya kutembelea Bonde la Ngorongoro.
????????????????????????????????????
Bonde la Olduvai Gorge ambako ni chimbuko la  historia ya binadamu ni kivutio cha kinachowavuta watalii wengi kutembelea eneo hilo.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga( wa kwanza kushoto)   akiteta jambo na Wakurugenzi wa Wizara hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea jana Makumbusho ya Olduvai Gorge
????????????????????????????????????
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi  akizungumza jana kwenye kikao cha Majumuisho  na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii mara baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea Bonde la Ngorongoro na Makumbusho ya Olduvai Gorge
              (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA –MALIASILI NA UTALII
…………………
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii  imeipongeza   Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  kwa kazi nzuri iliyofanya  ya ujenzi wa jengo la  makumbusho ya kisasa  katika Bonde la  Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya  Binadamu.
Kamati hiyo imesema imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo ambalo litawavutia watalii na wanasayansi  wabobezi wa masuala ya Malikale kutembelea Makumbusho hiyo.

Kamati hiyo ilibainisha kuwa   Makumbusho hiyo mbali ya   kutumika kuingiza pesa kupitia watalii pia  inatumika  kama kielelezo na utambulisho muhimu wa taifa  katika kutangaza utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi.
Hayo yalisemwa jana na Kamati hiyo  wakati ilipofanya  ziara ya kutembelea Ngorongoro Crater na  Makumbusho ya Olduvai Gorge  katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Kemilembe Luota ameipongeza Serikali pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuhakikisha kuwa  eneo la Olduvai Gorge linakuwa kivutio bora kwa ajili ya historia ya nchi na kivutio kikubwa cha Utalii duniani.
‘’ Sisi kama  Kamati tunaipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuyafanyia kazi mapendekezo yote tuliyoyatoa  kwa  mara ya kwanza tulipokuja kwa vile tumeona kazi nzuri imefanyika.’’
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea makumbusho hiyo  kwa vile idadi ya watalii wa ndani aliyokutana nayo sio ya  kuridhisha.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema makumbusho hiyo inatoa ushahidi dhahiri kuwa hata  wazungu, mababu zao walitoka Afrika.
Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Mtama,  Nape Nnauye amesema Makumbusho hiyo hadi hapo ilipofikia imeboreshwa kwa kiwango cha hali ya juu hata hivyo ameitaka Wizara ihakikishe inaitangaza ipasavyo ili watalii wengi zaidi wazidi  kutembelea.
Awali, Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, FredyManongi  amesema tangu kuzinduliwa kwa makumbusho hiyo kwa wiki moja  imekuwa ikipokea zaidi ya  watalii wapatao 40000 hali inayopekelea   kuwa ni miongoni mwa Makumbusho inayofanya vizuri zaidi barani Afrika

No comments :

Post a Comment