Kauli
hiyo imetolewa na washiriki wa mafunzo ya Elimu ya afya ya Uzazi na
Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendelea Micheweni, Kisiwani Pemba .
Wakichangia
mada ya afya ya Uzazi, iliyotolewa na Mkuu wa Elimu ya Afya Wilayani
Micheweni, Sulemani Faki Haji, mshiriki kutoka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali anayeratibu masuala ya Jinsia, Hidaya Khamisi amesema
kwamba takwimu za udhalilishaji za hivi karibuni zinaonesha Kisiwa cha
Pemba hususan wilaya ya Wete inaongoza kwa asilimia 70 kwa vitendo vya
ulawiti na ubakaji.
Kikundi
kazi cha wanafunzi na akina mama kikifanya zoezi la kuwapima uelewa wao
kuhusu somo walilopewa na malengo ya mafunzo hayo katika shule ya
Sekondari ya Chwaka Tumbe, Micheweni kisiwani Pemba.
Amesema vitendo hivyo vinasababisha fedheha katika jamii na kukatisha ndoto za mtoto kufikia malengo yake maishani.
Wakionyesha
ukubwa wa tatizo washiriki wamesema kuwa kwa hivi sasa si shuleni,
kwenye madrasa wala nyumbani ni mahali salama kwa watoto wa kiume na wa
kike kwani kwa sababu si ajabu kumwona mtu anayeheshimika katika jamii
hususan mzazi wa kiume akifanya mapenzi na watoto wake wa kuwazaa na
kuwapa mimba huku walimu wa dini kuwadhalilisha watoto.
Hivi
karibuni mkazi mmoja wa shehia ya Kiungoni Kimango, Hamad Omari Hamad
mwenye miaka 56 alikamtwa na polisi kutokana na vitendo vya ubakaji
alivyowafanyia watoto wake watatu akiwemo mtoto mdogo wa miaka minne na
mmoja wao kupewa mimba na baba huyo.
Kipindi
cha mazoezi cha kuendesha mahojiano kwa ajili ya kupata habari kati ya
Mtangazaji wa Redio Jamii Micheweni, Time Khamis na Mkuu wa Kitengo cha
Elimu ya Afya ya Kujamiiana na Uzazi wa Mpango Wilaya ya Micheweni,
Pemba Dk. Suleiman Faki Haji. Mahojiano hayo ni miongoni mwa vielelezo
katika mafunzo ya Elimu ya Kujamiiana na Uzazi iliyofanyika Micheweni,
Pemba yenye lengo la kuwapa ujuzi stadi wanafunzi wa shule nne za
sekondari na kikundi cha akina mama Wilayani Micheweni Kutayarisha
Vipindi vya redio vinavyohusu masuala yao.
Kwa
mujibu wa Mratibu wa Masuala ya Jinsia, Hidaya Khamisi, kuna mtandao
ujulikanao kama cheni ridhia unaendelea katika baadhi ya shule Kisiwani
Pemba wa watoto kwenda kufanya vitendo viovu iwe kupiga punyeto, kufanya
ngono au kulawitiana.
Utafiti
uliofanyika wilaya ya Wete mwaka 2016 kuhusiana na masuala ya
unyanyasaji wa watoto iligundulika kwamba darasa zima lenye watoto 60
walisema kwamba wanataka wawekewe mazingira ili wasidhalilishwe kwa
sababu watoto wote darasa hilo wamefanyiwa vitendo vya udhalilishaji
hususan kulawitiwa.
Picha
ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya Afya ya Kujamiiana na Uzazi
iliyofanyika Tarehe 18 hadi 23 Desemba 2017 katika shule ya Sekondari
Chwaka Tumbe, Micheweni kisiwani Pemba. Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na
Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Salma Khatib Mbarouk
(pichani mwenye gauni jeusi na kitambaa cheupe).
Aidha
ripoti nyingine kutoka shule moja wilayani Micheweni kwa mujibu wa
Meneja wa Kituo cha Redio Jamii Micheweni, Ali Kombo imeonyesha kwamba
kati ya wanafunzi 60 ni wanafunzi 10 tu ambao walikuwa bado
hawajafanyiwa udhalilishaji wa kingono.
Mafunzo
ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendeshwa na
UNESCO yana lengo la kuunda Vikundi vya Vijana Shuleni na Akina Mama
Watayarishaji Vipindi vya redio kwa kushirikiana na Redio Jamii
Micheweni, ambavyo vitasambaza Elimu rika kwa Vijana na Akina Mama.
No comments :
Post a Comment