Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na Wajumbe na Wenyeviti kwenye hafla
ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii nchini (TTLB)
vikijumuisha Bodi ya Leseni ya Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya
Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa
Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Saleh Pamba ( wa pili kushoto)
katika hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii
(TTLB) nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Naibu
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Alovce Nzuki, ( wa tatu kushoto)
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsias Mdamu, ( wa pili kulia)
Mjumbe wa Bodi ya TTLB, Michael Kamba (wa kwanza kushoto)
Mwenyekiti wa Bodi ya Leseni za
Biashara za Utalii Saleh Pamba ( wa pili kushoto) pm akizungumza na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia)
katika hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii
(TTLB) nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Naibu
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Alovce Nzuki, ( wa tatu kushoto)
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsias Mdamu, ( wa pili kulia)
Mjumbe wa Bodi ya TTLB, Michael Kamba (wa kwanza kushoto)
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufaa ya
Utalii, Balozi Mwanaidi Maajar akizungumza na Wajumbe na Wenyeviti
kwenye hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii
nchini (TTLB) vikijumuisha Bodi ya Leseni ya Biashara ya Utalii,
Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya Utalii zilizonduliwa
leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri
ya Utalii, Prof Wineaster Anderson akitoa neno la shukrani kwa Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kwa kuchaguliwa kuwa
Mwenyekeiti kwenye kamati hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa vyombo vya
kusimamia Biashara ya Utalii nchini (TTLB) vikijumuisha Bodi ya Leseni
ya Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa
ya Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe na Wenyeviti
waliochaguliwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia
Biashara ya Utalii nchini (TTLB) vikijumuisha ni Bodi ya Leseni ya
Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya
Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
Wajumbe na Wenyeviti kwenye hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia
Biashara ya Utalii nchini (TTLB) vikijumuisha Bodi ya Leseni ya
Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya
Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Lusungu Helela- MNRT
…………..
Wizara ya Maliasili na Utalii
imefanya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia biashara ya utalii nchini
katika Chuo cha Taifa cha Utalii kilichopo jijini Dar es salaam, ambapo
vyombo hivyo vimejumuisha kamati ya ushauri,Mamlaka ya rufaa pamoja na
Bodi ya mamlaka ya leseni.
Akiongea leo katika uzinduzi
huo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japheth Hasunga amewapongeza
wanakamati wote waliochaguliwa na kusema kuwa anaamini kuwa watafanya
kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuhakikisha kuwa sekta ya utalii
inapiga hatua kusonga mbele.
Pia, Naibu Waziri Hasunga
amesisitiza kuwa vyombo hivyo vya kusimamia biashara ni vyombo muhimu
sana katika kuendeleza sekta ya utalii na wajumbe wa vyombo hivyo ni
muhimu kwa kusimamia sekta ya utalii nchini.
“Ni vyombo muhimu sana katika
kuendeleza sekta ya utalii na wajumbe wa vyombo hivi ni muhimu sana kwa
kusimamia sekta ya utalii hapa nchini” amesema Hasunga.
Aidha, Hasunga ameiomba Bodi
ya Leseni ya Utalii iliyochaguliwa kufanya kazi katika misingi mikuu
mitatu ya utawala bora ambayo ni Uhuru, uwazi, usawa na uzalendo ili
kuepukana na migongano na kutokuelewana nyakati za kazi.
“Nawaomba mfanye kazi katika misingi ya utawala bora Uhuru, usawa, Haki na uzalendo”amesema Hasunga.
Katika hatua nyingiune, Naibu
Waziri Hasunga amesema kuwa sekta ya utalii ni sekta inayochangia
kiasi kikubwa pato la Taifa pia inasaidia upatikanaji wa fedha za
kigeni kwa urahisi, hivyo amewaomba watanzania kuwa wazalendo kwa
kuhamasisha uhifadhi wa mazingira pamoja na utamaduni wa mtanzania ili
vivutio vizidi kuwepo kwani wasipotunza mazingira utalii hautaendelea
kuwepo.
Pia amesema kuwa japo Tanzania
ina vivutio vingi vya utalii bado mapato ni madogo ukilinganisha na
vivutio vilivyopo hivyo ameeleza mikakati ya serikali kuwa imepanga
kufikia watalii milioni mbili mpaka ifikapo mwaka 2020 ambapo jukumu
hilo ni la kila Mtanzania.
“Mapato ni madogo ukilinganisha na
vivutio vilivyopo na serikali tumepanga kufikia watalii milioni mbili
ifikapo mwaka 2020 ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafikia idadi hiyo.
amesema Hasunga.
Pia ameisistiza Bodi ya leseni
ya utalii kuhakikisha leseni za biashara zinatolewa kwa wakati na kwa
kuzingatia kanuni, taratibu na sheria zilizopo.
“Mhakikishe leseni zinatolewa
kwa wakati sahihi bila kucheleweshwa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na
sheria kama inavyosema”amesema Hasunga.
No comments :
Post a Comment