Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China
hapa nchini Mhe. WANG Ke akimwelezea jambo Waziri wa Habari, Utamduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa hafla fupi ya
kukabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO)
iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo.
Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimsikiliza
Waziri Mshauri wa Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong walipokutana
katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya
Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini
Dar es Salaam leo. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za
ofisi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Waziri
Mshauri wa Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong wakitia saini hati
ya makabidhiano ya vifaa katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo
iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo.
Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akielezea jambo
mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (katikati) na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini
Mhe. WANG Ke walipokutana katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa
vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi
za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus. Msaada huo
unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi ya Krismasi
kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke
mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya Idara ya
Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Msaada huo unajumuisha
Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
No comments :
Post a Comment