Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha
uhamasishaji mbinu za kupambana na udunavu kwa watoto chini ya miaka
mitano kwa madiwani na watendaji kata. Wengine pichani ni Makamu
Mwenyekiti halmashauri hiyo, Mhe. Edward Shigela, Mwenyekiti wa
halmashauri, Mhe. Boniphace Butondo na Afisa Lishe Wilaya, Avelina
France.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo akifungua kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakiwemo
madiwani na watendaji kata wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika
katika ukumbi wa halmashauri.
Afisa Kinga na Uchanjaji Wilaya, Musa Doha akitoa mada kwa washiriki wa kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akichangia mada.
Mtoa mada kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii, Perpetua Kilalo akitoa mada kwa washiriki wa kikao hicho.
…………….
Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
imezindua mradi wa Mradi wa Mtoto Mwerevu unaotekelezwa na Serikali kwa
kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la IMA WORLDHEALTH, Pamoja
na Chuo cha Cornel.
Lengo kuu la mradi huo ni
kupunguza udumavu kwa asilimia 7 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano ambao unatekelezwa katika halmashauri 36 zilizo ndani ya mikoa
mitano ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,
Mhe. Boniphace Butondo amefungua kikao cha uhamasishaji mbinu za
kupambana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na
watendaji kata.
Imeelezwa mradi huo utasaidia
kuimarisha mikoa na halmashauri zake kwa kuzijengea uwezo wa watendaji
wake wa sekta zote zinazohusika na masuala ya lishe kuhusu kupanga na
kufanya ufuatiliaji wa shughuli hizo katika jamii.
Pia utachangia fedha za
utekelezaji kwenye bajeti na mipango ya mkoa na halmashauri 36 kwa njia
ya ruzuku ya uwajibikaji na kuhakikisha fedha zitakazotolewa
hazitaifanya mamlaka hizo za Serikali zisitenge fedha kwa ajili ya
masuala ya lishe.
Hivyo badala yake utahamasisha
ongezeko la bajeti ya shughuli za lishe kupanda katika kipindi chote cha
mradi huo unapoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu.
No comments :
Post a Comment