Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo(aliyeshika
fimbo) akipima kina cha KIsima kilitengenezwa kienyeji kwa ajili ya
kunyweshea mifugo katika eneo la Kafunjo Wilaya ya Missenyi Mkoani
Kagera leo. Waliomzunguka ni wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifana
Halmashauri ya Missenyi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo
(aliyenyanyua mikono) akiongea na wafugaji wa nchini Uganda leo baada ya
kufanya ziara ya kikazi katika eneo la Omwaarogwamabaare. Kushoto ni
Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Tanzania, bwana Richard Tumusiime
Kabonero kulia (anayecheka) ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Martin Ruheta. (
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo
(aliyenyanyua mkono)akimweleza jambo Balozi wa Uganda nchini Tanzania
Mhe.Richard Tumusiime Kabonero (kulia) walipokuwa katika ziara ya kikazi
leo kwenye Mto Kagera katika kijiji cha Kakunyu. Wengine kushoto kwa
Katibu Mkuu ni Dkt. Martin Ruheta Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kulia kwa Balozi ni Suleiman Ahmed saleh,
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo akiwa na
Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Tumusiime Kabonero
(Mwenye suti nyeusi) na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani
Athmani kwenye kikao cha kazi kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa kagera.
Picha na John Mapepele
…………….
Na John Mapepele –Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasilano, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (0784 441180)
Tanzania na Uganda leo
wamekubaliana kuunda mara moja timu ya pamoja ya wataalamu wa mifugo
itakayokuwa ikifuatilia hali ya mifugo ili kudhibiti milipuko ya
magonjwa hatari ya Mifugo.
Akizungumza leo mjini Bukoba
kwenye mkutano wa wataalam wa mifugo wa Tanzania na Uganda
ulioandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini, Balozi wa Uganda
nchini bwana Richard Tumusiime Kabonero amesema ushirikiano wa karibu
baina ya Tanzania na Uganda kwenye sekta ya mifugo siyo kitu cha
hiari bali ni jambo la laziima ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko
ambayo ni hatari kwa mifugo ya pande zote mbili.
Balozi Kabonero amesema njia bora
ya kudhibiti magonjwa ya wanyama ni kuwa na timu ya pamoja ya wataalam
watakaokuwa wakifuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini kila
wakati badala ya utaratibu wa sasa wa kila nchi kushughulikia peke
yake.
“Uganda kama ndugu wa karibu wa Tanzania tuna kila sababu ya kushirikiana ili kuboresha sekta hii” alisisitiza balozi Kabonero
Akizungumzia kwa upande wa
Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya
Mifugo, Dkt. Mary Mashingo amesema ushirikiano huo utasaidia kuboresha
huduma za mifugo baina ya nchi mbili kwa kuzingatia kuwa taaluma ya
udaktari wa mifugo imehuishwa na inadhibitiwa na bodi za taaluma hiyo
kidunia.
Aidha, amewataka wafugaji wa asili
kote nchini wabadili mitazamo ya kutegemea serikali katika kukuza
sekta badala yake washirikiane nayo ili kuharakisha mapinduzi ya sekta
ya mifugo.
“Bado kuna kazi ya kubwa ya
kufanya ili kuikwamua sekta, lakini pia tukiamua kwa pamoja baina ya
serikali na wafugaji nadhani tutakuwa na kipindi kifupi tu cha kufanya
mabadiliko makubwa kwenye sekta hii” aliongeza Dkt. Mashingo
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Uzalishaji Mifugo na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, bwana
Victor Mwita anasema kuwa kuimarika kwa minada itakayosimamiwa kisheria
katika mipaka ya nchi ya Tanzania na Uganda itasaidia kuongeza tija
katika sekta ya mifugo hapa nchini.
Aidha, Dkt. Mashingo alisisitiza
kwamba wafugaji wenyewe ndiyo wanaoweza kuifanya sekta kupiga hatua kwa
kuzingatia na kusimamia sheria mbalimbali za mifugo nchini. Alizitaja
baadhi ya sheria ambazo ni kipaombele kwa wafugaji kuzingatia kwa sasa
kuwa ni pamoja na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo namba 17ya mwaka 2003 na
Sheria za Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka
2010.
Akitolea mfano wa mafanikio
yaliyoletwa na wafugaji wenyewe nchini , Dkt. Mashingo alisema wafugaji
wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
wakati huo marehemu Joel Bendera waliweza kupunguza kwa kiasi kikubwa
migogoro iliyokuwepo baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Aidha alisema magonjwa kama
Ndigana kali (ECF ) kama ikitokomezwa kabisa yasaidia kuongeza idadi
ya mifugo nchini kwa kuwa ugonjwa huo ukiingia unachangia kuua 80%
ya ndama wanaozaliwa.
Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka 2010.
Akitolea mfano wa mafanikio
yaliyoletwa na wafugaji wenyewe nchini , Dkt. Mashingo alisema wafugaji
wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
wakati huo marehemu Joel Bendera waliweza kupunguza kwa kiasi kikubwa
migogoro iliyokuwepo baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Aidha alisema magonjwa kama
Ndigana kali (ECF ) kama ikitokomezwa kabisa yasaidia kuongeza idadi
ya mifugo nchini kwa kuwa ugonjwa huo ukiingia unachangia kuua 80%
ya ndama wanaozaliwa.
Akichangia katika kikao hicho
Mtendaji Mkuu wa Ranchi za Mifugo nchini(NARCO) Profesa Philemoni
Wambura alisema bado kuna mahitaji makubwa ya mifugo katika viwanda
vya nyama.
“Mahitaji halisi ya ng’ombe wa
kuchinjwa katika viwanda vyetu nchini ni 800 kwa siku lakini bado
hatujaweza kufikia lengo hilo. Tuna kazi ya kufanya “ alisisitiza
Profesa Wambura
Kaimu Mkurugenzi Idara za Huduma
za Mifugo katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Martin Ruheta amesema ili
sekta ya mifugo ifanikiwe lazima uzalishaji wa malisho uboreshwe malisho
yanachangia kwa asilimia 70 hadi 80 kwa ng’ombe wa maziwa na kwa
ng’ombe wa nyama inakwenda mpaka asilmia 90 Katika uzalishaji wa mifugo,
hakuna miujiza mingine na ndo maana nchi za wenzetu kama vile Brazil
wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta hii.
No comments :
Post a Comment