Sunday, December 3, 2017

WAZIRI KIJAJI AWATAKA WAHITIMU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji
ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza juzi katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu
Njiro Arusha ambapo pamoja na mambo mengine amewaonya wahitimu nchini
kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani
hawatabaki salama katika utawala huu. (Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
 Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha uhasibu
Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo ya chuo cha Uhasibu Arusha katika mahafali chuoni hapo juzi
 
Mkuu wa kitivo cha uhandisi,mazingira na Computer
Paul David Greening
kutoka Uingereza akizungumza katika mahafali yao juzi katika Chuo cha
Uhasibu NjiroArusha
Kushoto ni mgeni rasmi ambaye ni NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akisoma maelezo
mafupi ya chuo cha Uhasibu Njiro Arusha katika mahafli juzi chuoni hapo


 Wahitimu
wakifatilia mahafali hayo kwa ukaribu zaidi
 Meza
kuu wakiwa katika picha ya pamoja,wapili kushoto ni
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro,Dk.Faraji
Kasidi akiteta jambo
 Naibu  Waziri wa Fedha na
Mipango Dk.Ashatu Kijaji katika mahafali chuoni hapo juzi
Wanafunzi
waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakiwa katika picha ya pamoja
na mgeni rasmi
Baadhi
ya watumishi wa chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi juzi katika mahafali chuni hapo
 
Na Pamela Mollel,ARUSHA 
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji ametoa onyo kali
kwa  wahitimu wa Uhasibu nchini
kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani
hawatabaki salama katika utawala huu. 
Akizungumza juzi
katika mahafali ya 19 katika Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha, wakati
akitunuku vyeti vya ngazi mbalimbali viiwemo vya Uhasibu kwa wahitimu 1324,
Dk.Ashatu alisema baadhi ya wataalamu wa Uhasibu wanachangia kurudisha nyuma
Maendeleo kwa tamaa zao.
Alisema ni vema watumie
elimu waliopata kubuni ajira na pale watakaotoa ajira wafanye kwa weledi na
uadilifu.
Alisema endapo wataalamu
hao watabadilika na kuwa na uadilifu itawezesha Taifa kufanikisha ndoto yake ya
kufikisha uchumi wa Viwanda kabla ya mwaka 2025.
Aidha alipongeza Chuo
kuwa wabunifu wa kuongeza kozi kulingana na huhitaji wa jamii hadi kufikia 33 ikiwemo
ya Shahada mpya ya Kijeshi ilioanza kutolewa mwaka huu.
Kuhusu ombi la ujenzi wa
Hosteli na kumbi za Mihadhara, alisema serikali itazitatua kulingana na jinsi
wanapopata fedha,japo alishauri uongozi wa Chuo kuhakikisha sekta  binafsi
wanaona watawasaidiaje.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo
cha Uhasibu Njiro,Dk.Faraji Kasidi alisema mwaka huu wameadhimisha
Mahafali  ya 19 ya Chuo hicho na ya nane ya Chuo hicho Kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Coventry ya Uingereza.
Alishukuru serikali kwa
kutoa mikopo kwa nusu ya wanachuo wa mwaka wa kwanza 2017 na kufanikisha ndoto
kwa watoto maskini.
 

No comments :

Post a Comment