Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William (watatu kushoto) akikata
utepe wa Katiba ya Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) kuashiria
kuzinduliwa kwa chama hicho leo jijini Dar es Salaam,aliyeshika Katiba
hiyo (kulia) ni Rais wa PRST Bw.Loth Makuza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(kushoto) na Rais wa
Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) Bw.Loth Makuza (kulia)
wakionyesha Katiba ya chama hicho kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa
umma waliyohudhuria uzinduzi wa chama hicho (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(wanne
kushoto)akimkabidhi cheti Bw.Innocent Mungy kilichotolewa na uongozi wa
chama Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) kwa kutambua mchago
wake katika kuanzishwa kwa chama hicho mara baada ya uzinduzi wake leo
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha
Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus
William(aliyeketi wanne kushoto) mara baada ya uzinduzi wa chama hicho
leo jijini Dar es Salaam na watatu kutoka kulia) ni Rais wa PRST Bw.
Loth Makuza.
………………
Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam.
Idara ya Habari Maelezo pamoja na
Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) wametakiwa kuungana kwa
pamoja na kuandaa Kanuni za Maadili ya Taaluma ya Mawasiliano kwa Umma
kwa kuzingatia maslai ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Bw.Nicolaus William alipokuwa ...
akizindua chama cha PRST chenye
lengo la kuongeza ueledi kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa umma nchini
.
“Ningependa kuona chama hichi
kinakuwa mstari wa mbele katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanataaluma
wake kama lilivyolengo kuwa chama kitajikita zaidi katika kuongeza
weledi kwa wanatansia pamoja na kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika
sekta ya mawasiliano nchini kwa kulingana na mahitaji ya
soko,”Bw.William.
Akiendelea kuzungumza katika
uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa ni vyema wadau wote
wa taaluma ya mawasiliano kwa umma watambue umuhimu wa chama hichi
kwani wao ndiyo wenye dhamana ya kukikuza,kukiendeleza na kukijengea
misingi imara itakayodumu na kuleta tija ndani ya taifa.
Kwa upande wa Mwakilishi wa
Msemaji Mkuu wa Serikali kutoka Idara ya Habari Maelezo Bw.Jonas
Kamaleki alieleza kuwa serikali inaunga mkono jitihada za kuanzishwa kwa
PRST na iko tayari kutoa ushirikiano wakati wote.
“Serikali ingependa chama hichi
kuwa na mikakati madhubuti na utekelezaji wenye tija na hata kuwa mfano
kwa Afrika Mashariki bila ya kujali kuchelewa kwa kuanzishwa
kwake,”Bw.Kamaleki.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es
Salaam, Shule ya Habari na Mawasiliano kwa Umma Dkt.Dietrick
Kaijanangoma alitoa nasaha kwa Maafisa Uhusiano wa taasisi mbalimbali
nchini ya kuwataka kuwa wabunifu na kufanya tafiti ndogo na kubwa kwa
ajili ya kuimarisha taasisi zao na zaidi kujifunza kwenda na wakati kwa
kutambua mahitaji ya umma.
Pamoja na hayo nae Rais PRST
Bw.Loth Makuza alitoa shukrani kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania Awamu ya Tatu Mhe.Benjamin William Mkapa kwa kuanzisha
sekta ya habari nchini.
Halikadhalika Bw.Makuza alitoa
ombi kwa taasisi mbalimbali kuunga mkono uanzishwaji wa chama hicho
pamoja na wanataaluma kujitokeza kwa wingi na kujiunga na chama
utaratibu wa kujiunga unapatikana kupitia tovuti ya www.prst.or.tz.
No comments :
Post a Comment