Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Iringa
wakipita mbele ya Mkuu wa Chuo Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani
kwa ajili ya kutunukiwa vyeti vyao katika maadhimisho ya mahafali ya 20
ya chuo hicho siku ya Jumamosi Mkoani Iringa.
Wahitimu wa Shahada ya Sheria
(LL.B) katika chuo Kikuu cha Iringa wa kwanza kulia Richard Kipingu,
Charlotte A. Mwaigwisya(wa pili kulia) ,Msumi
Shabani(katikati),Catherine Eliwako Mjemah(wa pili kushoto) na Edwin
Mushi(wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
maadhimisho ya mahafali ya 20 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho siku ya
jumamosi Mkoani Iringa
Picha na Mpiga picha wetu.
……………..
Na Mwandishi Wetu Iringa
Mkuu wa Chuo Kikuu Iringa Jaji
Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani amewataka wahitimu wa chuo hicho
kufanyia kazi yale yote waliyojifunza darasani kwa kuzingatia maadili
ili kujenga taifa bora.
Akizungumza katika mahafali ya 20
ya Chuo hicho siku ya jumamosi MKoani Iringa Jaji Mkuu Mstaafu Ramadhani
alieleza kuwa taifa bora hujengwa kwa kuzingatia maadili mema.
“Taifa bora hujengwa kwa
kuzingatii maadili mema ambayo ni utii,heshima,kufuata sheria,kanuni na
taratibu za utendaji kazi kwa jamii husika “ alisema Jaji Mkuu Mstaafu
Ramadhani.
Aidha aliongeza kwa kuwataka
wanafunzi hao kuunga mkono juhudi za Seriklai ya awamu ya Tano chini ya
Uongozi wa Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha tunafikia
uchumi wa viwanda.
Naye Mhadhiri katika Kitivo cha
Sheria wa Chuo Hicho Bw. Renatus Mgongo amewahisi wahitimu hao kuwa
waadilifu katika utekelezaji wao wa majukumu ili kuleta matokeo chanya
kwa Taifa.
Katika mahafali hayo wahitimu
waliotunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na shahada
ya Uandishi wa Habari (35), Shahada ya Theolojia-Divinity (9), Shahada
ya Sheria (172), Shahada ya Utawala wa Biashara (110), Shahada ya Elimu
Katika Hisabati (82 na Shahada ya Ushauri Nasihi (58),
Wahitimu wengine walitunukiwa
Shahada ya Maendeleo ya Jamii (205), shahada ya Sayansi ya Technolojia
ya Habari-IT (30) na Shahada ya Athropolojia ya Utamaduni na Utalii
(139),
stashahada ya Theolojia (14), Cheti cha Utawala wa Biashara (88), Cheti cha Theolojia (12) na Cheti cha Sheria (6).
stashahada ya Theolojia (14), Cheti cha Utawala wa Biashara (88), Cheti cha Theolojia (12) na Cheti cha Sheria (6).
No comments :
Post a Comment