Mwenyekiti
wa Ukoo wa Patel, Harish Patel akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mfano wa
hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha zitatumika kwaajili ya kulipia
gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi
hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)Prof. Mohamed Janabi
akiwa katika picha ya pamoja na ukoo wa Patel pamoja na wafanyakazi wa
Taasisi hiyo mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi
22,500,000/= fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za
upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Ukoo
wa Patel ukiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mfano
wa hundi ya shilingi 22,500,000/= kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) fedha
ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa
watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Mkurugezi Mtendaji wa Taasisis ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi akongea na waandishi wa
Habari mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi shilingi
22,500,000/= na Ukoo wa Patel , fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya
kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika
Taasisi hiyo.
Picha na JKCI
………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Ukoo wa Patel umekabidhi kiasi
cha shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia
gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Akikabidhi fedha hizo leo
Mwenyekiti wa Ukoo huo Harish Patel alisema watoto wengi wanazaliwa na
ugonjwa wa moyo na wengi wao hawana fedha za kulipia matibabu wameona
kwa kidogo walichokipata kisaidie kulipa gharama za matibabu ya wagonjwa
hao.
“Kila wakati, kila mwaka
kutokana na kipato tunachokipata tumekuwa tukisaidia jamii katika mambo
mbalimbali ikiwemo elimu na afya na leo hii tumeona furaha zaidi
kusaidia watoto”, alisema.
Akipokea fedha hizo Mkurugenzi
Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliushukuru Ukoo wa Patel kwa
kuona umuhimu wa afya ya mtoto na kusaidia kulipia gharama za matibabu
na kuziomba Taasisi, Mashirika na watu binafsi wenye uwezo wajitokeza
kulipia matibabu ya watoto.
Prof. Janabi alimalizia kwa
kusema kuwa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni wengi kati
ya watoto milioni mbili wanaozaliwa asilimia moja (1%) wanazaliwa na
matatizo ya Moyo hivyo bado fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya
matibabu.
No comments :
Post a Comment