Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele akitoa maelekezo kwa
wakandarasi wa mradi wa uboreshaji usambazaji maji katika jiji la Dar es
Salaam wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya mradi huo leo.Kutoka
kushoto ni Makamu Rais wa Kampuni ya Jain Irrigation System Ltd ambao
ndiyo mkandarasi mkuu wa mradi huu Bw. Anil Vitankar, Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es Salaam (Dawasa)
Mhandisi. Romanus Mwang’ingo na Meneja Mradi wa Kampuni ya Wapcos Ltd
Mhandisi P. G. Rajan. Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es Salaam
(Dawasa) Mhandisi. Romanus Mwang’ingo akimuelezea Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele(kushoto)hatua zilizofikia katika
kutekeleza mradi wa uboreshaji usambazaji maji katika jiji la Dar es
Salaam wakati wa ziara ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya miradi hiyo
leo.Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja na
kushoto ni Meneja Mradi wa Kampuni ya Wapcos Ltd Mhandisi P. G. Rajan. Baadhi
ya wafanyakazi wakitandaza bomba katika eneo la Kibamba kama
walivyokutwa wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi
Isack Kamwele (hayupo pichani) kukagua maendeleo ya mradi huo leo jijini
Dar es Salaam. Waziri huyo amefanya ziara na kukagua ujenzi wa matenki
tisa katika maeneo ya Mabwepande, Salasala, Makongo/ Changanyikeni,
pamoja na ulazaji wa mabomba. Waziri
wa Maji na Umwagiliaji akikagua maungio ya bomba linalotandazwa katika
maeneo ya Kibamba alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi uboreshaji
usambazaji maji Dar es Salaam leo. Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele (katikati) akipewa
maelezo na Meneja Miradi wa Kampuni ya Wapcots Ltd Bw. P. G. Rajan
kuhusu ujenzi wa tanki la maji wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa mradi uboreshaji usambazaji maji Dar es Salaam leo.Kushoto
ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es
Salaam (Dawasa) Mhandisi. Romanus Mwang’ingo. Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wanajenga mradi uboreshaji
usambazaji maji Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo
ya mradi huu leo. (Picha na: MAELEZO)
Pages
Tuesday, December 5, 2017
Ujenzi Mradi Uboreshaji Mfumo wa Usambazaji Maji Dar Wafikia Asilimia 62
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es Salaam
(Dawasa) Mhandisi. Romanus Mwang’ingo (kushoto) akimuelezea Waziri wa
Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele hatua zilizofikia katika
kutekeleza mradi wa uboreshaji usambazaji maji katika jiji la Dar es
Salaam wakati wa ziara ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya mradi huu
leo.Kutoka kulia ni Mhandisi Godwini Mlay na Mtendaji Mkuu wa Dawasco
Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment