Mheshimiwa
Naibu Waziri aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya awamu ya
tano imeweka mkazo katika kukuza uchumi kupitia ujenzi wa viwanda.
…………………………………………….
Naibu
Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, amekutana na Mhe.
Muhannad Shehadeh, Waziri wa Nchi anaeshughulikia Uwekezaji kutoka
Jordan ambaye ameambatana na wafanyabiashara 40 kwa ajili ya kuangalia
fursa za biashara na uwekezaji nchini.
Katika
kikao hicho Mheshimiwa Naibu Waziri ameishukuru nchi ya Jordan kwa
kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri wa kisiasa na kiuchumi. Alimshukuru
Mheshimiwa Waziri wa Jordan kwa kuongoza ujumbe huo mkubwa wa
wafanyabiashara na alieleza kuwa ni imani yake wakati wa mkutano wa
pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania walioletwa pamoja na TCCIA
watapata fursa ya kushirikiana kwenye sekta mbalimbali za uwekezaji.
No comments :
Post a Comment