Saturday, December 9, 2017

SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU WA TANZANIA BARA, RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. MAGUFULI ATANGAZA MSAMAHA KWA FAMILIA YA BABU SEYA

Papii Kocha, maarufu kwa jina la mtoto wa mfalme ( kushoto ) akiwa na baba yake mzazi, Nguza Viking " Babu Seya "
Nguza Viking ( kulia ) akiwa na mwanaye Papii Kocha wakitumbuza gerezani.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli hii leo akihutubia katika sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara ametangaza kuwasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Akihutubia mamia ya Watanzania na wageni mbalimbali waliokuwa wamefurika katika uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, Rais Dkt. Magufuli pia ametangaza msamaha kwa familia ya Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya pamoja na mtoto wake Papii Kocha waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

No comments :

Post a Comment