Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifurahia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Geoffrey Kirenga
wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha
Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa, wengine ni
Mkurugenzi wa Mashamba na Mifugo Kiwanda cha, Rob Nethersole na
Mratibu wa SAGCOT Ofisi ya Waziri Mkuu, Girson Ntimba.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda
cha Kusindika Maziwa, Asas Diary Milk, Fuad Faraj, wakati alipofanya
ziara mkoani Iringa, kukagua viwanda vinavyofanya kazi na Kongani ya
Ihemi inayotekelezwa na Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Sehemu ya mitambo ya Kiwanda
cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa,
kiwanda hicho kinahitaji tani 7,000 za Soya kwa siku kwa ajili ya
uzalishaji lakini hadi sasa wanapata tani 2,000 kwa siku hivyo
kupelekea kiasi kingine kuagizwa kutoka nje ya nchi. Mpango wa
uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari umeanza kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wananchi wanufaike na fursa hiyo.
Sehemu ya mitambo ya Kiwanda
cha Kusindika maziwa, Asas Milk Diary mkoani Iringa, kiwanda hicho kina
uwezo wa kusindika lita 50,000 za maziwa kwa siku lakini kinapata lita
20,000 kwa siku. Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini
mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari umeanza kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wananchi wanufaike na fursa hiyo.
……………
Na.Mwandishi Maalum.
Katika
moja ya jitihada za kuhakikisha mafanikio ya mkakati wa kujenga Uchumi
wa Viwanda nchini serikali imeendelea Kuboresha mazingira bora ya
biashara kwa wawekezaji kwa kuendeleza kilimo ili kuchochea maendeleo
na sekta ya kilimo kupitia Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Akizungumza
baada ziara ya Kukagua shughuli za SAGCOT mkoani Iringa kwa kutembelea
kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku Silverlands na
kiwanda cha kusindika Maziwa cha Asas Diary Milk, Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora alifafanua kuwa
njia ya kuliwezesha Taifa kuwa na uchumi imara utakaohimili ushindani
katika masoko ya kikanda na kimataifa ni kuboresha mazingira ya
Uwekezaji.
“Tunaweka
mazingira wezeshi ya kisera na kisheria ili kuhakikisha ukuaji
endelevu wa kiuchumi katika sekta ya kilimo hasa kwa kuishirikisha sekta
binafsi na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, tunao Mpango wa SAGCOT
tunataka kutumia fursa hizi katika kilimo kukuza uchumi, tuondokane na
kilimo cha kujikimu na kuhamia kilimo biashara. Wawekezaji wanahitaji
kuona utayari wa wakulima ili wawekeze. Tukumbuke zaidi ya asilimia 70
ya malighafi za viwanda zinatokana na kilimo”, alisema Kamuzora.
Naye
Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa ,Wamoja Ayoub, alifafanua kuwa tayari
mkoa huo umeanza kupata mafanikio kwa utekelezaji wa SAGCOT mkoani humo
kwa wakulima kuweza kulimochenye tija , kuongeza thamani mazao yao na
kupata masoko ya uhakika.
“Kutokana
na ongezeko la matumizi sahihi ya pembejeo kumekuwa na ongezeko la tija
kwa mazao kutoka tani 2.2 za mahindi kwa hekta kwa msimu wa mwaka
2014/2015 hadi tani 2.7 za mahindi kwa hekta kwa msimu wa mwaka
2016/2017na Mpunga kutoka tani 3.2 kwa msimu wa mwaka 2014/2015 hadi
tani 4.6 kwa msimu wa mwaka 2016/2017”, alisema Wamoja.
Kwa
nyakati tofauti wawekezaji katika Kongani ya Ihemi, Mkurugenzi Mtendaji
wa Biashara Kiwanda cha kuzalisha Vifaranga na chakula cha kuku
Silverlands, Sean Johnson na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha
Kusindika Maziwa Asas Diary Milk, Fuad Faraj, walieleza kuwa ili
kuboresha mazingira ya uwekezaji na kupunguza gharama za kufanya
biashara, wameiomba serikali kufanya mapitio ya kodi hasa katika
uzalishaji wa bidhaa za viwanda.
Wawekezaji
hao walibainisha kuwa serikali itafanikiwa zaidi katika kuboresha
mazingira ya uwekezaji na biashara ikiwa kutaanzishwa kituo kimoja cha
kufanyia kazi “One stop Centre” kwa mamlaka zote za udhibiti,
usimamizi na uratibu wa shughuli hizo kwa Kongani ya Ihemi (Iringa na
Njombe).
Pia
walishauri serikali kuweka ruzuku katika mbegu za viazi na alizeti za
viazi mviringo na ili kuwezesha wakulima wadogo kumudu kununua mbegu
bora zitakazo ongeza uzalishaji na kuchangia malighafi za viwanda
vilivyo katika kongani ya Ihemi (Iringa naNjombe)
Awali, akieleza utekelezaji wa Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT),
Geoffrey Kirenga alieleza kuwa wanaendelea kuboresha ubia kati ya sekta
ya umma na sekta binafsi ili kuweza kuboresha mazingira bora ya
uwekezaji na biashara katika kongani ya Ihemi
“Tunaamini
kilimo ni fursa kwani ni wazi wawekezaji wanategemea kwa kiasi
kikubwa mavuno na mazao bora ili kuzalisha bidhaa nzuri. Uchumi wa
viwanda unategemea kilimo chenye tija na ninyi mnatuhakikishia kuwepo
tija hiyo.”
Programu
ya SAGCOT inatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro,
Iringa, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Njombe na Katavi na imegawanywa katika
kongani (cluster) sita za Ihemi (Iringa na Njombe), Rufiji, Kilombero,
Mbarali, Ludewa na Sumbawanga. Program hiyo imeanza kutekelezwa mwaka
2011 na mwisho wake mwaka ni 2030. WafadhIli wa SAGCOT ni Serikali ya
Tanzania, Shirika la misaada la Uingereza (UKAID), Shirika la misaada la
Marekani(USAID), Benki ya Dunia (WBG), Ubalozi wa Norway, Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na AGR.
No comments :
Post a Comment