Tuesday, December 5, 2017

RC GAMBO AWAASA WATAALAM WA UGAVI NA UNUNUZI KUZINGATIA UADILIFU KATIKA KAZI ZAO


image1
Mhe. Gambo akizungumza na wadau katika kongamano la nane la wataalam wa ugavi na ununuzi lililofanyika jijini Arusha wa muda wa siku mbili.
image2
Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dr. Hellen Bandiyo akizungumza katika kongamano la nane la wataalam wa ununuzi na ugavi lililohitimishwa jijini Arusha.
image3
Mhe Gambo akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa kongamano la nane la wataalam wa ugavi na ununuzi.
……………..
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewaasa wataalam wa ununuzi na ugavi kuzingatia maadili katika kazi zao za kila siku ili kuleta ufanisi katika maeneo wanayotumikia.
Bwana Gambo ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la nane la wataalam wa ununuzi na ugavi lililofanyika mkoani Arusha kwa muda wa siku mbili.

Awali akimkaribisha Mhe. Gambo kufunga kongamano hilo mwenyekiti wa PSPTB Sr. Dr. Hellen Bandiyo amemhakikishia mkuu huyo wa mkoa kwamba wao kama wataalam wa ununuzi wanao mchango mkubwa sana katika kuhakikisha malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kuelekea uchumi wa viwanda yanafanikiwa.
“Ni jukumu la wagavi kuzingatia maadili katika maeneo ambayo tumeaminiwa ili kumsaida rais wetu Dr. Magufuli kuweza kuifikisha nchi yetu katika uchumi wa viwanda, na sisi kama wataalam wan chi hii ni lazima tujione tuna deni katika ustawi wa chi yetu” alisema Dr. Bandiyo.
Mhe Gambo aliwaasa wataalamu hao kuhakikisha wanazingatia weledi na kuitumia taaluma yao vizuri kwa ustawi wa taasisi zilizowaajiri, “Taaluma ya ugavi na ununuzi ni zaidi ya kwenda dukani na kununua, inakwenda mbali zaidi ya hapo inahitaji weledi na uadilifu ili kuleta matokeo chanya katika maeneo yetu ya kazi kwa ustawi mzuri wa taifa letu” Mhe Gambo alisema.
Aidha moja kati ya changamoto alizozipokea Mhe Gambo ni pamoja na baadhi ya waajiri kuwatumia wataalam wa manunuzi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ambapo Mhe Gamboa amewataka kwa kuanzia wawasilishe orodha ya waajiri hao waliopo mkoani kwake ili aone namna ya kuwashughulikia kwa kua kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za nchi yetu.

No comments :

Post a Comment