Katika Picha, Ng’ombe aina ya
Borani inayomilikwa na muwekezaji kampuni ya Overland katika Ranchi ya
Mzeri , Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Katikati Waziri wa Mifugo na
Uvuvi. Mhe. Luhaga Mpina akiongea vyombo vya habari baada ya ziara ya
ukaguzi wa baadhi ya vitalu katika Ranchi ya Mzeri iyopo Wilayani
Handeni Mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin
Gondwe, na kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Overland Bw. Faizal Edha.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina kati kati na Mkuu wa Wilaya ya Handeni kulia Godwin Gondwe pamoja
na wataalam kutoka Wizarani na Mkoani Tanga wakiwa katika zoezi la
kukagua baadhi ya vitalu vilivyopo katika Ranchi ya Mzeri Wilayani
Handeni.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akikimkimbiza Ng’ombe aina ya Borani katika Ranchi ya Mzeri
alipokuwa katika zoezi la ukaguzi wa vitalu .
Aliyesimama Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akongea na Uongozi wa Wilaya ya Handeni na
wajumbe wa Msafara kabla ya kuanza kwa ziara katika Ranchi ya Mzeri.
……………
NA MWANDISHI MAALUM – HANDENI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhaga Mpina ameagiza kuvunjwa kwa mkataba ulioundwa baina ya RANCHI ya
Taifa NARCO na kampuni ya Overland kwa pamoja na kuunda kampuni ya
OVENCO uliyokuwa na mapungufu ya kisheria na kiutendaji kufunjwa ifikapo
mwisho wa mwezi huu wa December na kutoa mwezi mmoja kwa NARCO kuunda
mkataba mpya wenye mwengozo wa kisheria.
No comments :
Post a Comment