Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kulia) akimkabidhi mche wa sabuni
mmoja ya wafanyakazi wanaosafisha barabara na mitaa mbalimbali ya Mji wa
Dodoma mara baada baada ya kuzungumza na wafanyakazi hao katika Viwanja
vya Nyerere Mjini Dodoma jana. Mkurugenzi huyo aliwapatia wafanyakazi
hao wapatao 133 zawadi ya Shilingi 10,000 na Mche mmoja wa sabuni kila
mmoja ikiwa ni motisha hususan katika kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho
wa Mwaka.
Baadhi ya wafanyakazi wanaosafisha
Barabara na Mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma wakifurahia hotuba ya
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati
alipofanya nao mkutano katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana.
Mkuu wa Idara ya Mazingira na
Usafishaji Manispaa ya Dodoma Dickson Kimaro (kushoto) akizungumza
na wafanyakazi wanaosafisha barabara na mitaa mbalimbali ya Mji wa
Dodoma kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi
(katikati) kuzungumza na wafanyakazi hao. kulia ni msimamizi wa
wafanyakazi hao John Lugendo.
Wafanyakazi 133 wanaosafisha
barabara na mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma wakikabidhiwa Fedha taslim
Shilingi 10,000 na mche wa sabuni kila mmoja ikiwa ni zawadi ya motisha
iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin
Kunambi (hayupo pichani) jana katika Viwanja vya Nerere Mjini Dodoma.
Wanaokabidhi ni Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafishaji Manispaa ya
Dodoma Dickson Kimaro (wa pili waliokaa) na Afisa Mazingira ambaye ni
Msimamzi wa Wafanyakazi hao John Lugendo (wa kwanza waliokaa).
Sehemu ya wafanyakazi wanaosafisha
Barabara na Mitaa mbalimbali ya Mji wa Dodoma wakifuatilia hotuba ya
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati
alipofanya nao mkutano katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana.
Kando ni maboksi ya sabuni ambapo kila mmoja alizawadia mche mmoja na
fedha taslimu Shilingi 10,000 na Mkurugenzi huyo huku akiwaahidi
kuwakatia Bima ya Afya.
PICHA: RAMADHANI JUMA-OFISI YA MKURUGENZI
………………..
NA RAMADHANI JUMA,
OFISI YA MKURUGENZI
MKURUGENZI wa Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ameahidi kuwakatia Bima ya Afya
wafanyakazi 133 wanaosafisha mitaa na barabara zote za Mji wa Dodoma ili
wawe na uhakika wa matibabu wao na familia zao.
Alitoa ahadi hiyo jana alipofanya
mkutano na wafanyakazi hao katika viwanja vya Nyerere katikati ya Mji wa
Dodoma ambapo pia aliwapatia fedha taslimu Shilingi 10,000 na mche
mmoja wa sabuni kila mmoja kama zawadi kuelekea mwisho wa mwaka 2017.
Mkurugenzi Kunambi alisema kuwa,
yeye kwa niaba ya Uongozi wa Manispaa ametoa zawadi na ahadi ya
kuwakatia Bima ya matibabu baada ya kufurahishwa na uchapa kazi wao
unaopelekea mitaa na barabara za Mji kuwa safi na kupendeza muda wote.
“Hiki tunachowapa leo hakina
thamani yeyote kwa kazi kubwa mnayoifanya, bali ni kuonesha kuguswa
kwetu tu kama Manispaa…ninyi ni kundi maalum na ni wafanyakazi muhimu
sana” alisema Kunambi akizungumza na watumishi hao.
“Nimefurahi kukutana na kuzungumza
na ninyi kipindi hiki cha mwisho wa mwaka…nawaahidi mapema mwakani
Manispaa itawakatika Bima za Afya wote itakayomwawezesha kila mmoja
kutibiwa yeye na wategemezi wake watatu” alifafanua.
Kwa upande wao, wafanyakazi hao
ambao wengi wao ni akina Mama walimshukuru Mkurugenzi huyo kwa niaba ya
Manispaa kwa kuwajali licha ya kuwa wao ni watumishi wa kada ya chini na
wanaofanya kazi kwa mkataba isiyo ya kudumu.
“Tumefurahi sana leo Mkurugenzi
wetu umekuja kuongea na sisi na kutupa zawadi na fedha tena katika
kipindi cha Sikukuu za mwisho wa mwaka…umetujali sana na sisi
tunakuombea kwa Mugu”… alisema mmoja ya akia mama hao akimshukuru
Mkurugenzi wa Manispaa.
No comments :
Post a Comment