Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza katika kikao na wadau wa pamba kilichofanyika mjini
Shinyanga. Wengine picha ni kuanzia kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba.
Sehemu ya wakuu wa mikoa inayolima zao pamba wakifuatilia matukio katika kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
(katikati mwenye miwani) akifurahia wimbo na viongozi wengine mara baada
ya kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho. Wengine pichani kuanzia
kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,
Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,
Zainab Telack.
Wakuu wa wilaya za Shinyanga
ambazo ndizo miongoni mwa wakulima wa pamba, kuanzia kushoto ni Fadhil
Nkurlu (Kahama), Nyabaganga Taraba (Kishapu) na Josephine Matiro
(Shinyanga) na kulia pichani Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi
wakifuatilia matukio.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu ikiwa ni miongoni mwa wakulima wakubwa wa pamba,
Stephen Magoiga (mwenye kaunda suti aliyeshika karatasi) akifuatilia
matukio katika kikao hicho.
Sehemu ya wakuu wa mikoa
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye
kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akichangia katika kikao hicho cha wadau wa pamba.
Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi akichangia katika kikao.
Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akitoa neno katika kikao hicho.
………………
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Kishapu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuhakikisha zinasimamia
kikamilifu kilimo cha zao la pamba ili kiwe na tija.
Ametoa agizo hilo katika kikao
na wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga ambapo alizitaka
halmashauri hizo kuratibu shughuli za kilimo hicho kwa kuwapangia ratiba
maafisa ugani kuwatembelea wakulima kuwapa elimu.
Akizungumza katika kikao hicho
kilichoikutanisha mikoa zaidi ya 10 inayolima pamba aliwataka watendaji
wakuu wa halmashauri hizo kuhakikisha kila kata na kijiji kunawepo na
maafisa ugani ili wasimamie kikamilifu kilimo.
Majaliwa aliwataka maafisa
ugani waliopo katika halmashauri hizo kuwafikia wakulima mashambani ili
kuwapa elimu na kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu kilimo hususan
cha pamba.
“Tunataka kuhahakikisha pamba
inaleta heshima na inaongeza mapato ya mkulima mmoja mmoja na hata
taasisi zetu yaani halmashauri na mikoa zinaingiza mapato kupitia zao la
pamba hivyo kila mmoja awajibike,” alisisitiza.
Pia, aliagiza pia ziweke
mpango kazi wa namna ya kukiletea mafanikio kilimo hicho huku akisisi
kuwa na kwamba atafanya ziara kukagua akisema atataka apewe taarifa ya
maendeleo ya kilimo hicho.
Aidha alizitaka halmashauri
kuwa na takwimu za misimu ya pamba na ziwe zimehifadhiwa vizuri kwenye
kompyuta ili popote zikihitajika zipatikane kwa urahisi.
“Tumejipanga kusimamia zao la
pamba kwani awali uzalishaji haukuwa mzuri mkulima anatumia nguvu nyingi
sasa tutasimamia kikamilifu kuanzia maandalizi hadi masoko,” alisema
Majaliwa.
Katika hatua nyingine
aliwataka wadau wa kilimo cha pamba maarufu kama dhahabu nyeupe watimize
wajibu ili kukifanya kiwe na tija hivyo kuinua uchumi.
Majaliwa pia aliagiza wataalamu
kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kujipanga na kuelekeza kuhusu
dawa zilizo bora kwa ajili ya zao hilo na Bodi ya Pamba iwajibike
kufuatilia maendeleo yake.
Mkutano huo umewakutanisha pia
mawaziri wenye dhamana ya Kilimo, Dk. Charles Tizeba, Viwanda na
Uwekezaji, Charles Mwijage, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala,
wabunge, wakurugenzi wa halmashauri, taasisi za kilimo, wakulima na
wanunuzi wapamba.
PICHA ZOTE NA ROBERT HOKORORO
No comments :
Post a Comment