Miss Universe Tanzania (kushoto)
akizungumza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa JK Nyerere. Anayefuatia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Compass
Communication, Maria Sarungi na mwakilishi wa Shirika la Ndege la
Ethiopia.
……………
Na Mwandishi wetu
Dar
es Salaam. Miss Universe Tanzania, Lilian Erica Maraure amelalamikia
hatua ya majaji ya kutomuingiza hata katika hatua ya16 bora ya fainali
hizo richa ya kuongoza katika kura za mitandao.
Lilian
ambaye ni mtangazaji wa TBC international, alisema hayo mara
alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere alisema
kuwa miaka yote, warembo wanaongoza katika kura za mitandao upata nafasi
ya kuingia katika hatua ya fainali tofauti na mwaka wake.
Alisema
kuwa ameshangazwa hatua ya majaji ya kuwaingiza katika hatua ya 16 bora
warembo ambao kuwenye kura za mitandao hawafanya vizuri na kumuacha
wewe.
“Natambua
kuwa maamuzi ya majaji ni ya mwisho, lakini nahoji hatua iliyochukuliwa
ya kuacha kuingia hatua ya 16 bora na hata kwenye fainali pamoja na
kupigiwa kura nyingi sana na kuongoza,” alisema Lilian.
Katika mashindano hayo, Mrembo wa Afrika Kusini, Demi-Leigh Nel-Peters alitwaa taji hilo.
Pamoja
na matokeo hayo,Lilian alisema kuwa amepata uzoefu wa kutosha mbali ya
kupata mikataba kadhaa ya kufanya maonyesho ya mavazi na ofa ya kusoma
nchini Marekani.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi ambaye pia ni
mratibu wa Taifa wa mashindano hayo, alisema kuwa wanayachukulia matokeo
hayo kama changamoto na kuangalia zaidi mashindano yajayo.
“Ni
kweli kuwa matokeo yanashangaza, hatujawahi kulalamika katika
mashindano ya nyuma, safari hii tulihamasisha wadau watupigie kura
nyingi, lakini matokeo ndiyo kama yalivyokuwa,” alisema Maria.
No comments :
Post a Comment