Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara
baada ya kutembelea Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya
siku moja, Leo Novemba 1, 2017. Picha Zote Na
Mathias Canal
Mathias Canal
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe katika
ukumbi wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya
Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo
Novemba 1, 2017.
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi
yaliyohifadhiwa kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya
siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ya
namna ya ununuzi na uhifadhi wa mahindi kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa
Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati
wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
…………………………………………………………………………….
Na Mathias Canal, Njombe
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa amesifu juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha
Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.
Mradi huo utahusisha ujenzi Wa
Vihenge vya kisasa, Mghala ya kisasa pamoja na ukarabati Wa Ofisi ambapo
baada ya mradi huo kukamilika wakala utakuwa umeongeza uwezo Wa
kuhifadhi Shehena ya mahindi ya uzito Wa zaidi ya Tani 250,000 ambapo
Vihenge vya kisasa ni 190,000 MT na Maghala 60,000 MT.
Mradi huo unataraji kutekelezwa
na kampuni mbili za kandarasi kutoka serikali ya Poland (Feerum na Unia
Arab) kwa usimamizi Wa Wakala Wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo unataraji
kugharimu zaidi ya Bilioni 150 za Kitanzania.
Tayari maandalizi ya awali
yameshakamilika ikiwemo Utiwaji saini mikataba, Uchunguzi Wa udongo,
Tathmini ya athari ya Mazingira, Pamoja na kutembelea eneo la mpango
kazi.
Akizungumza wakati akikagua Ghala
la Kuhifadhia mahindi Kanda ya Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa
Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alisema kuwa Wakala Wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) umefanya kazi kubwa ya ubunifu na kujiongeza
kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima katika Kanda zote saba ikiwemo ya
Makambako-Njombe, Kipawa-Dar es salaam, Dodoma, Shinyanga, Arusha,
Songea na Sumbawanga.
Alisema kuwa pamoja na Kanda ya
Makambako kupangiwa kununua jumla ya Tani 6500 katika msimu Wa mwaka
2017/2018 ambapo baada ya lengo kukamilika ziliongezwa fedha za ununuzi
hivyo kununua jumla ya Tani 8,961.530
Akisoma taarifa ya Wakala Wa
Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA)
Bi Vumilia L. Zikankuba alisema kuwa Kanda ya Makambako ni miongoni kwa
Kanda itakayoongezewa uwezo Wa kuhifadhi ambapo tayari kuna kiwanja
chenye ukubwa Wa Hekari 2,9965 kilichopo Makambako na Mbozi chenye
ukubwa Wa Hekari 53.691.
Alisema Wakala umefanikiwa
kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kununua baadhi ya Mazao ya
Chakula cha ziada kutoka kwa wakulima, Kutoa Chakula cha ziada kwa
waathirika, Kutekeleza mkakati Wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini
(MKUKUTA) kwa kutoa bei nzuri kwa wakulima wanaouza Mazao yao kwa NFRA
sambamba na utekelezaji Wa malengo ya milenia 2025.
Katika ziara hiyo ya kikazi ya
Siku Moja katika Mji Wa Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Kilimo
pia amekutana na kufanya kikao cha kazi na wafanyakazi Wa Wakala Wa
Taifa wa Hifadhi ya chakula Kanda ya Makambako ambapo pamoja na mambo
mengine amewasihi kufanya kazi kwa Nidhamu, Weledi, Kujituma, Uvumilivu,
Bidii na mshikamano.
Wakati huo huo amefanya
mazungumzo na wakulima kutoka Kanda ya Makambako ambapo wakulima hao
wamesifu Juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Wa
Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali
ikiwa ni pamoja na kupunguza Tozo na Ushuru.
Wakulima hao kwa nyakati tofauti
wameupongeza Uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya
Makambako kwa kuwashirikisha na kuwajali wakulima katika kila hatua ya
ununuzi Wa mazao.
No comments :
Post a Comment