Saturday, December 23, 2017

MATENGENEO MAKUBWA MASHINE NAMBA MOJA YA KUFUA UMEME KIDATU YAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 95 KUKAMILIKA


 Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),
wakishirikiana na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia, wakifanya matengenezo makubwa ya mashine namba moja ya kufua umeme, kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro Desemba 22, 2017. Kituo hicho kina jumla ya mashine 4 (Turbines) za kufua umeme wa Megawati 204.

NA
 
Alisema.
Naye
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Power
Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, umeme unaozalishwa kutokana na
maji ni wa bei nafuu na kupongeza juhudi za serikali katioka kuhakikisha
wananchi wanatunza mazingira ili kutunza vyanzo vya maji ambayo hutumika
kuzalisha umeme.

“Tunaishukuru
sana serikali kwa hatua inazochukua kama kuboresha upatikanaji wa maji kwa
kutunza vyanzo vya maji (mazingira), hususan bonde la Mto Rufiji, timu
iliyoundwa na Makamu wa Rais ambayo imefanya kazi nzuri nahuenda baada ya muda
matokeo mazuri tutayaona.” Alisema.

Akifafanua
zaidi alisema, juhudi zinazofanywa na serikali kuongeza vyanzo vya kuzalisha
umeme kwa kutumia vyanzo vya maji kama vile Stigler
Gorge
zitasaidia sana nchi yetu na hii inaonyesha serikali ilivyodhamiria
kupunguza gharama za umeme kwa wananchi kwa vitendo.” Alisema.

Kwa
upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Bi. Leila Muhaji, amesema Shirika
limekuwa karibu na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji na vituo vya
umeme ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutunza mazingira ili
kunusuru vyanzo vya maji.

“Na
ushirikiano wetu na wananchi uko katika maeneo mbalimbali kama vile kutoa
huduma za afya bure kwa wananchi wanaoishi jirani na vituo vyetu vya kufua
umeme, shule za awali lakini pia hata usafiri yumekuwa tukiwapatia usafiri wa
bure wananchi ambapo hutumia magari yetu ya wafanyakazi kwenda maeneo jirani na
vituo.
Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine turbines kwenye bwawa la Kidatu mkoani Morogoro

 Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
  Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
 Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kulia), akizungumza kuhusu kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu, mkoani Morogoro. Katikati ni Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.
 Mhandisi Ikwasa, (kulia), akibadilishana mawazo na Afisa Mazingira wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bw. Yusuf Kamote.
 Geti la kupitishioa maji Kidatu.
 Meneja wa Kituo cha kufua umeme Kidatu mkoani Morogoro, Mhandsi Anthony Mbushi (kushoto), akifafanua masuala ya kiufundi kwenye chumba cha udhibiti umeme kilichoko chini ya ardhi kwenye Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
 Maafisa wa TANESCO na baadhi ya wahariri wakiangalia mashine iliyoharibika, a,mbayo kwa sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
Wasimamizi wa chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini wakati walipotembelewa na wahariri wa vyombo vya habari Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
Peter Rauya, (kushoto) na Senorina Maganga  wa chumba cha udhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini.
Wahariri wakipatiwa maelezo na maafisa wa TANESCO kuhusu utendaji kazi wa mashine za kufua umeme (Turbines) kituom cha Kidatu.
Waharorio wakiangalia mashine iliyoharibika ambayo sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
Mameneja wa vituo vya kufua umeme kutoka mikoani wakiwa kwenye kituo cha kufua unmeme Kidatu mkoani Morogoro. Mameneja hao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (wapili kushoto), akiwa na baadhi ya Mameneja wa vituo vya kufua umeme vilivyoko mikoani ambao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
Wasimamizi wa chomba cha udhibiti mifumo ya umeme cha Kidatu mkoani Morogoro; kutoka kushoto ni Peter Rauya, Senorina Maganga na Nicomedy Mhina.
Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda (kushoto), akiwa sambamba na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar ya Croatia wakati wakiendelea na matengenezo hayo.
Sehemu ya kuingilia “mgodini” chini ya ardhi kwenye mitambo ya kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro.

No comments :

Post a Comment