Thursday, November 2, 2017

ZAIDI YA SH. 24 ZAOKOLEWA KWA SERIKALI KUSHINDA MASHAURI YALIYOKUWA YAKIHUSISHA MADAI YA FEDHA

3


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Mdemu aliesimama akiwsilisha taarifa ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 ya ofisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma.
16
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi  katikati akiangalia nyaraka mbalimbali mezani wakati alipokutana na kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake kwa Kamati hiyo mjini Dodoma
5
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katba na Sheria Mhe. Mohamed Mchengerwa katikati akitabasamu baada ya kumsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Kabudi wakati alipokutana na watendaji wa Taasisi za Wizara waliokuwa wakiwasilisha taarifa za utekelezaji wa taarifa hizo
………………..
Serikali  imeokoa kiasi cha Shilingi Bilioni 24,556,724,598 na Dola za Marekani  7,817,170.48 kupitia mashauri ya madai ambayo Serikali ilishinda yaliyoendeshwa katika ...
mahakama mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali   Bw. Gerson Mdemu alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya ofisi yake kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokutana mjini Dodoma.
Amesema wameiwezesha Serikali  Kushinda kesi kwenye mashauri 23 yaliyokuwa yanahusisha madai ya fedha na kuongeza kuwa kama Serikali isingekuwa makini na kushindwa kesi ingelipa kiasi cha shilingi 24,556,724,598 na na Dola za Marekani  7,817,170.48.
“Kama Serikali isingekuwa makini na kushindwa kesi ingelipa kiasi cha shilingi 24,556,724,594 “Hivyo basi kwa kushinda kesi hizo, Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 24,315, 498,042.44 na Dola za Marekani  7,817,170.48 na hivyo kupoteza kiasi cha shilingi 241,226,557.56, kwa kesi ilizoshindwa”, alifafanua.
Amesema ofisi yake imeendelea kutekeleza kikamilifu jukumu lake la kutoa ushauri wa kisheria kwa serikali na Taasisi zake na na kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile mradi ya bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga ambayo italeta ajira na kuchangia mapato kwa Serikali.
Amesema Ofisi yake pia imeendesha mashauri 169 ya kikatiba yakiwemo mashauri mapya 37 , mashauri hayo yote yapo katika hatua mbalimbali ambapo Mashauri 25 yalihitimishwa na kufanya kubaki mashauri 144 ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi .

No comments :

Post a Comment