Naibu Waziri mhe. Zhao Dacheng
akizungumza aliesimama kulia akizungumza wakati alipotembelea Shule Kuu
ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi akizingumza wakati alipotembelea Shule Kuu ya Sheria
ya Chuo Kikuu cha Dar es salaaam pamoja na mgeni wake Naibu Waziri wa
Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng.
Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo
Kikuu cha Dar es salaaam Prof. Hamudi Majamba akizungumza mbele ya Naibu
Waziri wa Sheria wa China Mhe. Zhao Dacheng alipotembelea Chuo Kikuu
cha Dar es salaaam
Naibu Waziri wa Sheria wa China
mhe. Zhao Dacheng wa tatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu Dar es salaam
alipotembelea chuo hicho
…………….
Naibu Waziri wa Sheria wa China Mhe. Zhao Dacheng ametembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaaam.
Waziri Dacheng aliambatana na mwenyeji wake Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.
Katika ziara hiyo Waziri huyo wa
China alipata fursa ya kujifunza jinsi Shule hiyo ya Sheria
inavyotekeleza jukumu la kutoa msaada wa kisheria kwa umma wa watanzania
wenye uhitaji.
Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha
Dar es salaam imekuwa ikitoa huduma ya msaada wa kisheria nchini kupitia
walimu wao wenye vyeti vya uwakili, wanafunzi wake wa mwaka wa pili, wa
tatu , wanne na wale ambao wanasubiria kujiunga na Taasisi ya mafunzo
kwa vitendo
Waziri huyo wa China yuko nchini
kwa ziara ya siku nne ambapo anatembelea taasisi mbalimbali
zinazojihusisha na utoaji wa msaada wa sheria kwa watu wenye uhitaji
nchini.
No comments :
Post a Comment