Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (kulia) akizungumza na Waandishi wa
Habari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika makabidhiano
ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya dharura 114
yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo tarehe
29/11/2017
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (katikati), akipokea msaada wa
simu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Aitel Tanzania Bi. Beatrice
Singano (kushoto), katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika
kwenye namba ya dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini
Dar es Salaam leo tarehe 29/11/2017
Kamishna wa Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akizungumza na
Waandishi wa Habari, Maafisa wa Zimamoto na Uokoaji na Wafanyakazi wa
Airtel, katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye
namba ya dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es
Salaam leo tarehe 29/11/2017
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (Kulia), Kamishna wa Operesheni
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage (kushoto) na Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano (katikati) wakishika
kipeperushi kinachoonyesha namba ya dharura 114 ya Jeshi. katika
makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya dharura
114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo tarehe
29/11/2017
Picha ya Pamoja, Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa pili kulia)
akiwa na Maafisa waandamizi wa Jeshi hilo pamoja na Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa tatu kulia),
katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya
dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo
Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji
………………..
Airtel Tanzania imetoa msaada wa
simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambazo zitatumika kwa ajili ya
kurahisisha na kuimarisha mawasiliano ya namba ya
dharura 114 wakati wa
kutoa taarifa za dharura za moto na majanga mbalimbali nchini.
Simu hizo zimetolewa kwa Mikoa yote ya Jeshi la Zimamoto ambapo wateja wa Airtel watapiga bure ilikupata huduma za Jeshi hilo.
Akikabidhi simu hizo, Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema wao kama
Airtel wanatambua umuhimu wa Jeshi hilo na wanaamini kuwa wananchi sasa
wataweza kupata huduma za Jeshi hilo kwa urahisi kupitia namba hiyo ya
dharura.
“Airtel tunatambua umuhimu wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika jamii, hivyo tunaamini utoaji wa
taarifa za majanga kwa wakati muafaka unarahisisha shughuli za uokoaji
na kuzuia kwa kiwango kikubwa hasara ambayo inaweza kusababishwa na
majanga hayo katika jamii” alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa Upande wake Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Thobias Andengenye aliishukuru
Kampuni ya Airtel kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania
Beatrice Singano kwa msaada huo wa simu na kusema utaimarisha utendaji
wa Jeshi hilo.
Wateja wa Airtel sasa wataweza
kupata huduma kwa haraka baada ya kupiga simu. “Tunashukuru sana na tuna
imani kuwa wateja wa Airtel sasa watakuwa na urahisi wa kutufikia
kupitia namba 114, tofauti na hapo nyuma” alisema Kamishna Jenerali wa
Jeshi hilo
Natoa rai kwa wananchi kuendelea
kutumia vema mitandao ya simu kwa kutolea taarifa za kweli na si
vinginevyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mwananchi yeyote
atakayetumia vibaya mawasiliano ya kimtandao, hasa kwa kuitumia vibaya
namba ya dharura 114 inayotumiwa na wananchi kutolea taarifa za matukio
ya moto, maokozi na majanga mengine.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
No comments :
Post a Comment