Baadhi ya wananchi na wadau wa
maendeleo wakiwa katika maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club
Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah
Kairuki akinyajua bango juu lenye ujumbe unaosema “Ukatili wa Kijinsia
Unachelewesha Tanzania ya Viwanda” wakati akipokea Maandamano maalum ya
ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika
viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah
Kairuki akiwaasa wadau na watanzania kujikita katika kupambana na
ukatili wa kijinsia wakati akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es
Salaam Novemba 25,2017.
Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akieleza
namna Wizara inavyoshikiana na wadau na wananchi kupambana kuondoa
ukatili wa kijinsia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club
Dar es Salaam Novemba 25,2017.
Mkurugenzi wa Shirika la WILDAF
Tanzania Dkt Judith Odunga akitoa salamu kwa niaba ya wadau katika
ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
uliofanyika katika viwanja vya Leade’s Club Dar es Salaam Novemba
25,2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah
Kairuki(kulia) akiteta jambo na Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(kushoto)
wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia uliofanyika katika Viwanja vya Leader’s club Kinondoni Dar es
Salaam Novemba 25, 2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah
Kairuki akisaliamiana na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Nchini Bw.
Alvaro Rodriguez wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es
Salaam Novemba 25,2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah
Kairuki akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Balozi wa Marekani nchini
Bi Inmi Patterson wakti wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es
Salaam Novemba 25,2017.
Baadhi ya wadau na wananchi
wakifuatlia hotuba ya Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki(hayupo
pichani) aliyemwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika
ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba
25,2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah
Kairuki (watatu kushoto waliokaa )na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(katikati
waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja wadau na waharakati wa kupinga
vitendo vya ukatili wa kijinsia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku
16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leade’s
Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
………………………………………………………………………………
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Watanzania wametakiwa kutumia
nguvu zao katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ili
kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Madini Mhe. Angellah Kairuki alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan katika ...
ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.
Mhe. Angellah Kairuki amesema
kuwa kimsingi kiwango cha ukatili wa kijinsia nchini na dunia bado ni
kubwa na kwa mujibu wa Taarifa ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria
vya Malaria Tanzania ya mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa wanawake 4 kati
ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa
miaka 15.
Ameongeza kuwa takwimu zinonesha
kuwa asilimia 42 ya wanawake waliowahi kuolewa wamekumbana na ukatili wa
wenza wao ama wa kimwili,au ukatili unaohusisha ngono.
“Nawaomba watanzania wenzangu
katika maeneo yenu pazeni sauti na kufanya kwa vitendo kupinga masuala
ya ukatili wa kijinsia unaowakumba sana wanawake na watoto” alisema Mhe.
Angellah.
Aidha kwa upande wake Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt
Faustine Ndugulile amesema kuwa athari za ukatili wa kijinsia ni kubwa
sana katika Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja
na taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa kampeni hii ya
Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hasa ilenge kuinua uelewa wa
jamii na wadau mbalimbali kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na
watoto.
“Kampeni hii imekuja wakati
muafaka na kwakuwa tatizo la ukatili wa kijinsia hapa nchini bado ni
kubwa basi itasaidia kulitatua kwa jitihada za pamoja za Wadau na
Serikali” alisema Mhe. Dkt. Ndugulile.
Naye Mkurugenzi wa WILDAF
Tanzania Dkt. Judith Odunga ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wao
katika kupambana na ukatili wa kijinsia na kuomba kufanyiwa kwa
marekebisho ya baadhi ya Sheria ili ziende sambamba na kupinga ukatili
wa kijinsia nchini.
Siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia uadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 10 na
kwa mwaka 2017 Kauli mbiu inasema FUNGUKA! Ukatili Dhidi ya wanawake na
Watoto haumwachi Mtu Salama: CHUKUA HATUA!
No comments :
Post a Comment