Naibu Waziri wa Sheria wa China
mhe. Zhao Dacheng akiwa katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es salaam.
Mhe.Dacheng na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya siku nne.
Naibu Waziri wa Sheria wa China
mhe. Zhao Dacheng watatu toka kulia na ujumbe wake wakiwa katika ukumbi
wa mikutano jijini Dar es salaam
Waziri wa Katiba na
Sheria Prof.Palamagamba Kabudi wa pili kushoto akizungumza na ugeni
wa Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng katika ukumbi wa
mikutano jijini Dar es salaam
Waziri wa Katiba na
Sheria Prof. Kabudi aliekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja
na Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng wa pili kushoto
wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini
Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi akimkabidhi zawadi ya Kinyago mgeni wake Naibu Waziri
wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng ambaebyuko nchini kwa mwaliko wa
Prof Kabudi.
………………..
Tanzania na China wamekubaliana
kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali kama njia mojawapo ya
kupambana na uhalifu wa kimataifa ambao umekuwa ukiisumbua dunia.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada
ya kufanyika mazungumzo kati ya ...
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi na mgeni wake Naibu Waziri wa China mhe. Zhao Dacheng
ambae yuko nchini kwa ziara ya siku nne nchini.
Akizungumza baada ya kukamilika
kwa mazungumzo hayo, Prof.Kabudi ameyataja makosa ya kimataifa ambayo
wamekubaliana kuwa ni makosa ya kimtandao,utakatishaji fedha,
usafirishaji binadamu na mengineyo ambayo yamekuwa yakiikabili dunia kwa
wakati huu.
Prof.Kabudi pia amesema kwamba
wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kayika eneo la msaada wa kisheria
kwa watu wenye uhitaji ambapo China pia watajifunza kutoka kwa Tanzania
katika eneo hilo ambalo Inataka kuwa na sheria yake kama ilivyofanya
Tanzania.
Viongozi hao pia wamekubaliana
kushirikiana katika eneo la mafunzo ili kuwaongea ujuzi na uwezo
watendaji wao kupitia semina za kimataifa au mafunzo maalum ili
kubadilidhsna uwezo na uzoefu katika eneo la usimamizi wa sheria nchini.
Tanzania na China pia
wamekubaliana kushirikiana katika eneo la Mahakama ikiwa ni pamoja na
usimamizi na uendeshaji wa Magereza nchini.
Awali akizungumza katika kikao
hicho Naibu Waziri wa China Mhe. Dacheng alisema Tanzania ni moja ya
nchi marafiki wa dhati wa China urafiki ambao uliasisiwa na viongozi
waandamizi wa nchi hizo.
Alisema ziara yao nchini inafungua
milango mipya ya ushirikiano baina ya China na Tanzania na kuongeza
kuwa itazidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.
Amesema anaamini kuwa Wizara yake
imedhamiria kuisaidia Tanzania katika sekta ya Sheria ili isonge mbele
kama ilivyofanikiwa China na kuongeza kuwa wao pia wataitumia nafasi
hiyo kujifunzakatima maeneo ambayo Tanzania imepiga hatua kama eneo la
msaada wa sheria kwa watu wake.
Naibu Waziri huyo wa Sheria wa
China yuko nchini kwa mwaliko wa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania
Prof. Kabudi, anatarajiwa kutembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chio Kikuu
chabDar es salaam na Chama cha Wanasheria Tanganyika na Desemba Mosi
ataelekea visiwani Zanzibar ambako atakutana na Jaji Mkuu wa Tanzania na
viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
No comments :
Post a Comment