Naibu
Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (mwenye koti)
akifuatilia majadiliano baada ya kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Wakala
wa Meli wa Taifa mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu
kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini
Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Prof. Norman Sigalla King
(katikati) akichangia maoni yake kuhusu Muswada huo. Wa kwanza Kulia ni
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Selemani Kakoso.
Mjumbe wa
Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania Mzee Renatus Mkinga (aliyesimama)
akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu
kuhusu Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli wa Taifa kwenye kikao
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma. Naibu
Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (mwenye koti)
akifuatilia majadiliano hayo na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mhe. Prof. Norman Sigalla King.
Mjumbe wa
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Rukia Kassim akichangia
maoni yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli wa Taifa mbele ya
Kamati hiyo na wadau wa sekta ndogo ya usafiri wa majini kwenye kikao
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imewasilisha Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma.
Muswada huo umewasilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Prof. Makame Mbarawa.

Wakati
akiwasilisha Muswada huo, Mhandisi Nditiye alisema kuwa Muswada huu
unapendekeza kutungwa kwa Sheria itakayoanzisha Shirika la Uwakala wa
Meli ambalo pamoja na majukumu mengine litakuwa na jukumu la kutoa
huduma ya uwakala wa meli na kudhibiti huduma za usafiri na usalama wa
vyombo vya majini.
Ameongeza kuwa, Muswada huu utaweka mfumo madhubuti wa uendeshaji wa biashara ya uwakala wa meli na udhibiti wa huduma za usalama wa usafiri wa meli hivyo utaimarisha udhibiti wa sekta ndogo ya usafiri wa meli na kuifanya sekta hii kuchangia vyema katika uchumi na kuongeza pato la Taifa.

Muswada
huu ni moja ya jitihada za Serikali za kuhakikisha kuwa taasisi zake
zinajiendesha kwa faida, kibiashara, kwa ushindani na kutoa gawio kwa
Serikali ili iweze kuhudumia wananchi kwa kujenga miundombinu ya kisasa
na kuwapatia wananchi huduma mbali mbali za kijamii.
Mhandishi Nditiye aliyataja majukumu ya Shirika kuwa ni pamoja na uhakiki wa shehena inayoingia na kutoka kupitia bandari za Tanzania, uondoshaji shehena za madini, makinikia, wanyama hai, nyara za Serikali, na bidhaa zinazotokana na madini na udhibiti wa watoa huduma katika sekta ndogo ya usafiri majini, usalama wa meli na mazingira ya bahari.
Muswada huu utaipa mamlaka Shirika ya kutekeleza Sheria ya Bahari ya Mwaka 2003, kufanya ukaguzi wa meli za kigeni na udhibiti wa meli zilizosajiliwa Tanzania, udhibiti wa vivuko vya kibiashara, kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji, kudhibiti, kuratibu na kulinda mazingira ya bahari, kuainisha utaratibu wa kutoa na kuhuisha leseni na udhibiti wa ada na tozo. Pia, Muswada huu unaainisha taratibu na sifa za kampuni binafsi inayostahili kupewa leseni ya uwakala wa meli.

No comments :
Post a Comment