Na Dotto Mwaibale, Chato
WAKULIMA Wilaya Chato mkoani Geita wamefurahia mbegu bora ya mihogo, mahindi na viazi lishe waliopewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kuanzisha mashamba darasa ya mbegu hizo na kuzisambaza kwa wakulima wengine katika maeneo mengine.
Wakizungumza wilayani hapa leo kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu hizo katika vijiji vya Kibehe, Ipandikilo, Kitongoji cha Kaseni, Kijiji cha Itale na Bukiliguru kilichopo Kata ya Bwanga walisema mbegu hizo walizokabidhiwa na COSTECH kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo ni mkombozi kwao.
Ofisa Kilimo wa Kata ya Kachwamba, Hamisi Matesi alisema Costech kuwapelekea wakulima mbegu hizo itawasaidia sana kupata chakula wananchi wa kata hiyo ziada watauza.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho alisema wakulima walikuwa wakipata mavuno machache ya mahindi na mihogo kwa kuwa hawakuwa na mbegu bora hivyo baada ya kufunguliwa kwa shamba darasa la mbegu hizo katika maeneo yao wanategemea kupata mazao mengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari aliwataka wananchi hao kutambua kuwa mpango huo wa serikali ya awamu ya tano unawategemea sana wakulima katika kilimo hivyo fursa hiyo walioipata ya kupelekewa mbegu hizo wasiipoteze.
“Hakikisheni mbegu hizi bora za mihogo mnazopewa mnazitunza ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo hiki kupitia shamba darasa hili ili kila mkazi wa Chato aweze kulima na kuzalisha kwa tija” alisema Mhandisi Hari.
Hari ameishukuru COSTECH kwa kuamua kuipatia wilaya hiyo mashamba darasa katika vijiji hivyo kwani anaamini mbegu hizo zitasimamiwa vizuri na kisha kuwafikia wakulima wengi zaidi ili waweze kuachana na mbegu zao za zamani ambazo zinashambuliwa na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha matunda ya tafiti hizo yanawafikia walengwa.
Alisema mbegu hizo walizozikabidhi ikiwamo ya mahindi yanayostahimili ukame ya Wema 2109 zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato katika mihogo.
Dk. Bakari aliwataka wakulima hao kuyatunza mashamba darasa hayo na kubwa baada ya muda mfupi watarudi kuangalia maendeleo yake.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari
Msangi (kushoto), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akimkabidhi mbegu ya viazi lishe kwa
ajili ya shamba darasa la Kijiji cha Kibehe, Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari wakati wa uzinduzi wa shamba hilo
wilayani Chato leo. WAKULIMA Wilaya Chato mkoani Geita wamefurahia mbegu bora ya mihogo, mahindi na viazi lishe waliopewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kuanzisha mashamba darasa ya mbegu hizo na kuzisambaza kwa wakulima wengine katika maeneo mengine.
Wakizungumza wilayani hapa leo kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu hizo katika vijiji vya Kibehe, Ipandikilo, Kitongoji cha Kaseni, Kijiji cha Itale na Bukiliguru kilichopo Kata ya Bwanga walisema mbegu hizo walizokabidhiwa na COSTECH kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo ni mkombozi kwao.
Ofisa Kilimo wa Kata ya Kachwamba, Hamisi Matesi alisema Costech kuwapelekea wakulima mbegu hizo itawasaidia sana kupata chakula wananchi wa kata hiyo ziada watauza.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho alisema wakulima walikuwa wakipata mavuno machache ya mahindi na mihogo kwa kuwa hawakuwa na mbegu bora hivyo baada ya kufunguliwa kwa shamba darasa la mbegu hizo katika maeneo yao wanategemea kupata mazao mengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari aliwataka wananchi hao kutambua kuwa mpango huo wa serikali ya awamu ya tano unawategemea sana wakulima katika kilimo hivyo fursa hiyo walioipata ya kupelekewa mbegu hizo wasiipoteze.
“Hakikisheni mbegu hizi bora za mihogo mnazopewa mnazitunza ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo hiki kupitia shamba darasa hili ili kila mkazi wa Chato aweze kulima na kuzalisha kwa tija” alisema Mhandisi Hari.
Hari ameishukuru COSTECH kwa kuamua kuipatia wilaya hiyo mashamba darasa katika vijiji hivyo kwani anaamini mbegu hizo zitasimamiwa vizuri na kisha kuwafikia wakulima wengi zaidi ili waweze kuachana na mbegu zao za zamani ambazo zinashambuliwa na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha matunda ya tafiti hizo yanawafikia walengwa.
Alisema mbegu hizo walizozikabidhi ikiwamo ya mahindi yanayostahimili ukame ya Wema 2109 zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato katika mihogo.
Dk. Bakari aliwataka wakulima hao kuyatunza mashamba darasa hayo na kubwa baada ya muda mfupi watarudi kuangalia maendeleo yake.
Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiandaa shamba lao la mbegu.
Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiwa kwenye uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe na mihogo.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi wa Wilaya ya Chato, Monica Mulongo akizungumzia vitamini A inayopatikana kwenye viazi lishe ambayo ni muhimu kwa watoto.
No comments :
Post a Comment