Waziri Mpina katika Picha akivua samaki aina ya kambale alipotembelea Mradi wa mabwawa ya samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akiiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misenyi mara
baada ya zoezi la kutaifisha ng’ombe.
Katika Picha ni sehemu ya ng’ombe
6638 waliotaifishwa na serikali baada ya kuingia nchini kinyemela kutoka
nchi jirani ya uganda ng’ombe hao wanasubiri maamuzi ya Mhakama kwa
ajili ya Kupigwa mnada.
Aliyeshika Samakai aina ya Sato ni Waziri Mpina alipotembelea Mradi wa Mabwawa ya Samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.
…………….
NA; MWANDISHI MAALUM MISENYI
Akiwa katika muendelezo wa ziara
zake za oparation kamata mifugo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga
Mpina Ameagiza kukamilisha taratibu za Uhamiaji na Mahakama kupitia
mwanasheria mkuu wa Serikali wa Wilaya ya Misenyi Pamoja na Uhamiaji,
ili kuweza kupigwa mnada kwa idadi ya ng’ombe 6648 walioingia nchini
kinyemela toka ...
nchi jirani ya Uganda na kukamatwa.
Waziri mpina alisema uvamizi wa
kundi kubwa kama hilo la wanyama linaweza kusabisha madhara makubwa
katika mazingira kama vile mmomonyoko wa ardhi, kuharibifu wa vyanzo vya
maji, kumaliza malisho ya mifugo iliyoko nchini, kusababisha migogogoro
ya mara kwa mara kwa wakulima na wafugaji na hata kuleta maambukizi ya
magonjwa ya wanyama.
“Sisi kama Serikali hatuwezi
kuruhusu hali hii iendelee na mimi kama Waziri Mwenye dhamana nina
jukumu la kuhakikisha tunalinda lasimali hii ya malisho” Alisema Mpina.
Mpina alisema suala hili
haliingiliani na Ushirika wa Afrika Mashariki kwani Ushirika huo upo
kisheria hivyo wavamizi wanaoingiza mifugo kinyemela nchini toka nchi
jirani ni wahalifu kama wahalifu wengine.
“Kwa hiyo naangiza ng’ombe hawa
6648 waliokamatwa hatua ziendelee na ambao hawajakamatwa wakamatwe na
wataifishwe na Serikali.”Alisisitiza Waziri Mpina.
Kwa upande wa upande wake mkuu wa
Wilaya ya Misenyi Kanali Denis Mwila alisema kuwa zoezi la kutathmini
ng’ombe katika wilaya yake bado linaendelea na taratibu za kisheria
zinafuatwa.
Alipokuwa Mkoani Kagera Mapema Leo
Mpina alitembelea mabwawa ya mradi wa samaki yaliyopo Wilayani Muleba
katika kijiji cha Luhanga na kusema Serikali ina nia ya kukomesha
kabisa uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wavuvi haramu kule
waliko na kuwa na nyenzo.
Aidha, akiwa Bukoba Mjini Mpina
alitembelea kiwanda cha kuchakata samaki cha Suprime Fish Ltd na kuagiza
wamiliki wa viwanda vya samaki nchini kuhakikisha wanachukua hatua za
haraka kufufua viwanda hivyo na kuongeza uzalishaji kwani Serikali
imeshaanza kuchukua hatua ya kuhakikisha samaki wanapatikana kwa wingi
nchini.
No comments :
Post a Comment