Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua nyaraka
mbalimbali alipotembelea Kiwanda cha China Paper
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua kiwanda cha China Paper Corporation.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akizungumza katika
kiwanda cha China Paper Corporation.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akizungumza na
wafanyakazi wa shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM).
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akisikiliza
malalamiko ya wafanyakazi wa shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM).
………………
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde leo amefanya ziara
ya ukaguzi wa masuala ya kazi na kusikiliza kero na changamoto
mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.
Mavunde alianza ziara hiyo katika
shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM) ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi
na kutoa maagizo kwa Menejimenti ya ...
Uongozi wa Shule hiyo kutoa
mikataba kwa wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya
Ajira na Mahusiano kazini kinavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kuagiza
Taasisi za Serikali kuchunguza malalamiko juu ya unyanyasaji kwa
wafanyakazi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa menejimenti.
Naibu Waziri Mavunde amewaagiza
Afisa Kazi Mfawidhi na Afisa wa Uhamiaji wa mkoa wa Kilimanjaro
kuzichukua hati za kusafiria za raia wa kichina 9 mpaka
watakapowasilisha Vibali vya kufanya kazi nchini na Vibali vya makazi.
Aidha Mavunde alitembelea Kiwanda
cha China Paper Corporation ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na
kuiagiza Menejimenti ya Kiwanda hicho kuhakikisha sheria za Kazi
zinafuatwa kwa kutoa Mikataba kwa wafanyakazi wote na kuhakikisha haki
za wafanyakazi zinalindwa ikiwemo usalama wa mazingira ya kufanyia kazi.
Pamoja na maagizo hayo kwa
kiwanda,Naibu Waziri Mavunde aliwataka wafanyakazi nao kutimiza wajibu
wao na kutumia njia sahihi za malalamiko yao bila kuvunja sheria za
nchi.
No comments :
Post a Comment