Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa
kupewa Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo
hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao
katika kusimamia miradi ya JICA.
Balozi wa Japan nchini Mhe.
Masaharu Yoshinda (kushoto) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale Tuzo ya Rais wa
JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa
watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia
miradi ya JICA.
Balozi wa Japan nchini Mhe.
Masaharu Yoshinda (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa mara baada ya
kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango
yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika
la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) na Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) wakifutilia hafla ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale mapema wikiendi hii.
Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango
yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS
Mhandisi Patrick Mfugale akionyesha Tuzo ya Rais wa JICA katika hafla ya
kukabidhiwa tuzo hiyo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Kutoka
kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshinda, Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Makamu wa Rais
wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Toshio
Nagase.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS
Mhandisi Patrick Mfugale akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa
wafanyakazi wenzake Bi. Beatrice Kosongwa wakati wa hafla ya kumkabidhi
Tuzo ya Rais wa JICA iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es
Salaam. Kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu
Yoshinda, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa, Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA
nchini Tanzania Toshio Nagase.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
…………………………………………………………………
Na Ismail Ngayonga- MAELEZO
SERIKALI ya Japan kupitia Shirika
la Maendeleo la Kimataifa la nchi hiyo (JICA) imesema itaendelea
kuisadia miradi mikubwa ya maendeleo nchini ikiwemo barabara ili
kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa katika...
kuwaletea maendeleo
wananchi wake.
Hayo yamesemwa mwishoni wa wiki
Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati
wa utoaji tuzo ya heshima ya Rais wa JICA kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale.
Balozi Yoshida alisema tangu
mwaka 1980, JICA imekuwa mshirika wa karibu wa maendeleo na Serikali ya
Tanzania ikiwemo kuunga mkono juhudi za kukuza uchumi na kupunguza
umasikini kwa wananchi kupitia ufadhili wa miradi ya kipaumbele kwa
ikiwemo barabara.
Aliongeza kuwa utoaji wa Tuzo ya
Rais wa JICA kwa Mhandisi Mfugale imedhirisha imani ya Serikali ya Japan
kwa Tanzania katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo
inayofadhiliwa JICA, na kuahidi kuendelea kuimarisha uhusiano na
ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi wa Mataifa hayo.
“Misaada ya JICA nchini
unajumuisha misaada bila masharti, misaada ya kiufundi, kufadhili miradi
kwenye maeneo ya vipaumbele kwa serikali hususan katika sekta za
kilimo, miundombinu ya barabara, maji, nishati, utawala na afya” alisema
Balozi Yoshida.
Akizungumzia kuhusu tuzo ya Rais
wa JICA kwa Mhandisi Mfugale, Balozi Yoshida alisema tuzo hiyo hutolewa
kama alama ya utambuzi wa heshima kwa wataalamu, wataalamu washauri na
wafanyakazi wa kujitolea walifanikisha maendeleo katika nyanja za
raslimali watu na maendeleo ya miundombinu katika nchi zinazoendelea
ikiwemo Tanzania.
Balozi Yoshida alisema tuzo hiyo
imetolewa kwa Mhandisi Mfugale kutokana na mchango wake katika maendeleo
ya miundombinu inayounganisha mikoa mbalimbali nchini pamoja na nchi
jirani na kueneza ujuzi wake kwa wasaidizi waliomzunguka.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema tuzo ya
Mhandisi Mfugale imetoa somo kwa Wahandisi vijana wanaopaswa kuzingatia
miiko inayoongoza taaluma ya uhandisi nchini.
Aidha Prof. Mbarawa aliishukuru
JICA kwa utekelezaji wa miradi ya barabara nchini hususani katika
jitihada zake za kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia uchumi wa kati
kupitia uimarishaji wa miundombinu imara ya barabara.
“Uadilifu na uaminifu ni jambo la
msingi sana katika taaluma ya uhandisi, ni misingi mikuu iliyoonyeshwa
katika utendaji kazi Mhandisi Mfugale hadi anatunukiwa tuzo hii,
niwahimize wahandisi vijana muige mfano huu” alisema Waziri Mbarawa.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale alisema
tuzo aliyopewa ni zawadi kwa Serikali hususani wafanyakazi wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambao amekuwa akifanya nao kazi kwa
katika kutekeleza majukumu yake.
No comments :
Post a Comment