Tuesday, November 21, 2017

NUKUU YA MAMBO 19 YALIYOZUNGUMZWA KWENYE KIKAO CHA NEC IKULU LEO


index
Mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema (BAVICHA),Patrobas Katambi amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katambi ametangaza kujiondoa Chadema leo Jumanne Novemba 21,2017 katika mkutano wa halmashauri kuu ya CCM unaoendeshwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam.
Mbali na Katambi makada wengine wa CHADEMA wameamua kurudi CCM.
index
Wajkili Albert Msando akipongezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati alipotangaza kurejea CCM kwenye mkutano wa NEC unaofanyika Ikulu leo chini ya Uenyekiti Rais JPM.
…………………………………………………………………………………….
1. “Waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali ni 3004 na nafasi za wanaohitajika ni nafasi 201” – JPM
2. “Tulifanya magaeuzi makubwa ili kukirejesha chama kwa Wanachama na kurejesha imani ya CCM kwa Watu” – JPM
3. “Mageuzi haya yamekuwa miiba mikali kwa waliozoea kukichezea chama chetu” – JPM
4. “Kila siku Watu wanarejea CCM, ni ishara ya kupendwa vilivyo kwa CCM” – JPM
5. “CCM inahitaji viongozi wanaochukizwa na rushwa, uonevu, ubadhilifu. Wanaopenda kutimiza ahadi za TANU” – JPM
6. “Wajumbe msije na majina yenu mifukoni, mnaweza kurudi nayo yakiwa huko huko mifukoni” – JPM
7.  “Nina imani na uchambuzi uliofanywa na Sekretariet. Kwa wale ambao hawataridhishwa na mgombea yeyote, nimekuja na mafaili ya wagombea wote nitamwonyesha” – JPM
8. “Hapa ni kwenu, bila ya nyinyi (Wajumbe) nisingefika hapa.  Mna kila sababu ya kufanya kikao hapa” – JPM
9. “Katika siku za hivi karibuni tumeona mapinduzi ya kiutawala, kiitikadi, kiuchumi” – Dk. Mkumbo
10. “CCM ndio chama pekee kinachoonekana kina nguvu hapa nchini” – Dk. Mkumbo
11. “Nimekubali kurudi kwa dhati, ninaomba ridhaa nirudi mnipokee” – Lawrence Masha
12. “Nimerudi zizini nikiwa na mkia, nipo tayari kutumika” – Lawrence Masha
13. “Yale tuyotarajia Wapinzani tuyaone yakifanyika, yanafanyika katika utawala wako Rais Magufuli, tuna kila sababu ya kukuunga mkono” – Samson Mwigamba
14. “Kadri wanavyopiga kelele, ndivyo wewe unazidi kupanda mlima” – Samson Mwigamba
15. “CCM ni chama kinachoonyesha kuwajali watu, mimi kama kijana ninajivunia kuwa Mwanachama wa CCM” – Alberto Msando
 16. “CCM kilihaidi kupambana na umaskini, kutengeneza ajira, kurudisha nidhamu na uwajibikaji. Tuna kila sababu ya kupongeza kwa haya mambo mazuri” – Alberto Msando
17. “Leo hii nasaliti ubinafsi, umimi kwa kuamua kujiunga na CCM” – Patrobasi Katambi
18. “Upinzani wa leo unajadili mambo binafsi na matukio kuliko kujadili namna ya kulisaidia Taifa” – Patrobas Katambi
19. “Kijana ndani ya upinzani ni karai linalojenga ghorofa. Karai huonekana takataka baada ya ghorofa kukamilika” – Patrobasi Katambi

No comments :

Post a Comment