Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amegawa mashine 31 za aina mbalimbali
kutoka kampuni ya HiTECH International kwa vikundi 31 katika jimbo lake
la Dodoma Mjini. Mashine alizozitoa Naibu Waziri ni pamoja na mashine
za kutotolea vifaranga (incubators- mayai 1056 na mayai 528) mashine za
matofali (umeme na manual), mashine za Popcorn zenye matairi, vyerehani,
mashine za kutengeneza chaki (chaki 50,000-80,000 kwa siku), mashine za
kunyonyolea kuku mpaka kuku 500 kwa siku. Mavunde ametoa mashine hizo
zenye thamani ya milioni 55.8 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi
yake katika uvhaguzi wa mwaka 2015 kuwezesha wananchi ili wajikomboe
kiuchumi lakini pia kuunga mkono mpango wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa vikundi mbalimbali vya
Dodoma Mjini. Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akizungumza
jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde wakati wa hafla ya kukabidhi mashine
31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment