Baadhi ya wanafunzi waliofuzu masomo yao
wakiwa katika kusherekea mahafari yao. Mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF ukiwa
mojawapo ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kwa sasa unatoa mkopo wa elimu"Kamata Madigrii na GEPF" kwa
mwanachama yeyote aliyesajiriwa na mfuko huu, ili kusaidia kukuza maendeleo ya
kijamii na ya kiuchumi nchini.
Na Christian Gaya
Elimu ni nyezo muhimu katika maisha ya
binadamu. Kutokana na nguvu ya elimu katika kukuza uchumi wa nchi, mataifa
mengi duniani yaliyopata maendeleo ya kijamii na kiuchumi yamewekeza katika
sekta ya elimu. Hakuna taifa lolote duniani ambalo linaweza kupata maendeleo
bila watu wake kuwa na ...
elimu na kwa maana hiyo hakuna maendeleo bila elimu.
Elimu ndiyo inamfanya binadamu kuwa daktari,
rubani, mhandisi na mtaalamu katika nyanja mbalimbali. Kwa kutambua hilo
uwekezaji katika sekta hiyo umekuwa ukiongezeka. Leo hii kumesikika vilio vingi
nchini vikilenga mazingira bora na fursa zaidi katika sekta ya elimu
vinavyotokana na watu wengi kutambua nguvu ya elimu kwa vizazi vijavyo.
Wengi wenu ni mashahidi kuwa miongoni mwa
changamoto kubwa ambayo watu wengi wajasiriamali wanaopenda kujiajiri
wanakumbana nayo ni ukosefu wa mitaji na mikopo yenye masharti nafuu. Taasisi
nyingi za fedha nchini na benki za biashara zinatoa mikopo kwa riba kubwa na masharti
mengi, ambayo watu wengi hawawezi kuyamudu.
Kulingana na yakwimu za matokeo ya utafiti wa
nguvukazi na ajira ya mwaka 2005/2006, zinaonesha kuwa watu milioni 2.3
walikuwa hawana Ajira. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 5.8 ya watu wote nchini.
Kwa upande wa Jiji la Dar es Salaam, asilimia 31.4 ya watu wenye uwezo wa
kufanya kazi walikuwa hawana kazi.
Vilevile, kwa mujibu wa takwimu za hivi
karibuni zinaonesha kuwa wastani wa nguvukazi hasa vijana wasomi wanaotafuta
ajira kwa mwaka ni takriban laki nane hadi milioni moja. Hata hivyo, Ajira
rasmi zinazopatikana nchini katika sekta ya umma na sekta binafsi ni kidogo,
takriban ajira 80,000 hadi 100,000 kwa mwaka.
Pamoja na mafunzo ya ujasiriamali
yanayotolewa, kwa vijana na wazee wanatakiwa kuwezeshwa na kuwekewa mifuko ya uwezeshaji
yenye utaratibu maalum ulio wazi na mwepesi wa kupatikana kwa mikopo yenye riba
nafuu kama vile inayobuniwa na mifuko ya sekta ya hifadhi ya jamii Tanzania
Na ndiyo maana mfuko wa mafao ya kustaafu
GEPF kama mfuko wa hifadhi ya jamii umeamua kuwa na mkopo wa elimu "Kamata Madigrii na GEPF" kwa
mwanachama yeyote aliyesajiriwa na mfuko wa mafao ya kuustaafu wa GEPF
aliyeajiriwa katika sekta ya umma au binafsi na ambaye angependa kujiendeleza
kielimu kuanzia ngazi ya cheti, diploma, shahada ya kwanza na ya pili mpaka
shahada ya udaktari
Mwanachama wa GEPF anayetaka kukopa aina hii
ya mkopo anatakiwa awe amepata nafasi katika chuo husika, awe ameruhusiwa na
mwajiri kujiunga na masomo husika, awe amechangia katika mfuko kwa kipindi
kisichopungua miaka miwili, na mwisho ni kwamba mwanachama anatakiwa kurejesha
kupitia makato ya mshahara wake kwa kipindi cha kati ya miaka miwili mpaka
miaka mitano.
Faida za mkopo huu wa elimu kwa wanachama wa GEPF ni
kwamba wanapata fursa ya kuanza kunufaika na matunda ya uanachama wake akiwa
kazini na mwanachama kupata fursa ya
mkopo wenye riba nafuu na masharti nafuu na kinga ya bima dhidi ya majanga
Utafiti unaonesha ya kuwa zaidi ya 1,000 ya
wanachama wameanza kunufaika na huduma hii ya mkopo wa elimu na idadi kubwa
ikiwa rika ya vijana nchini.
Mwandishi wa makala hii ni mwanzilishi wa
Kituo cha HakiPensheni, mshauri na mtaalamu wa masuala ya pensheni. Kwa maelezo
zaidi gayagmc@yahoo.com unaweza kutembelea
tovuti hakipensheni monitor
online na hakipensheni blog +255 655 13 13
41
No comments :
Post a Comment