Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira (kushoto) Mh. Antony Mavunde (Mbunge), akimkabidhi mshindi wa 14 wa mchezo wa tatu Mzuka Bw. Robert A. Changadiko(45), hundi ya shilingi milioni sitini , Mjini Dodoma.
Mshindi wa droo ya 14 ya Tatu Mzuka Bw.Robert A. Changadiko (kulia)aliyejishindia donge nono la shilingi milioni sitini wiki hii, akiwa na rafiki yake bwana Bw. Daudi Mwangoto (katikati), ambaye alizawadiwa shilingi milioni moja kutoka katika promosheni ya cheza na washkaji shinda na washkaji ya Tatu Mzuka, kushoto ni Bw.Edwin Kawito ni mshindi wa Tatu Mzuka droo ya kumi (10) aliyejishindia shilingi milioni sitini.
Mshindi wa shilingi milioni sitini kutoka kijiji cha Msembata (Dodoma)Bw.Robert A. Changadiko mwenye umri wa maika 45, ambaye ni fundi minara,akifurahia ushindi wake.
NA MWANDISHI WETU
Naibu
Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mheshimiwa Anthony Mavunde leo
amemkabidhi kitita cha shilingi Milioni 60 mshindi wa droo ya Tatumzuka
Bwana Robert Changadiko ambaye... alijishindia kiasi hicho katika ‘Jackpot’
ya wiki hii katika droo ya kusisimua iliyoonyeshwa siku ya jumapili
kupitia vituo vya runinga kote nchini.
Bwana
Changadiko ambaye anafanya kazi kama fundi minara mjini Dodoma
alielezea furaha yake juu ya ushindi huo ambao hakuutegemea na
akaishukuru Tatumzuka kwa kutimiza hitaji lake la pesa wakati alipokuwa
akizihitaji zaidi.
"Niliamua
kucheza Tatu Mzuka kutokana na matatizo niliyokuwa nayo ya kifedha
ambapo nilihitaji fedha za haraka ili kukidhi mahitaji hayo. Kwakweli
nina furaha kubwa sana na nashukuru kwamba nilijaribu bahati na
ikatimia” alisema.Mavunde alimpongeza mshindi kwa kushinda kiasi hicho
na Tatu Mzuka kwa ajili ya kuendelea kutengeneza mamilionea na
kubadilisha maisha ya watu.
"Ninakushauri
kwamba kabla ya kuanza kutumia pesa yako,tenga muda kufikiri namna
utakavyotumia fedha yako ili utimize malengo yako na ili pesa
uliyojishindia ilete mabadiliko ya kweli katika maisha yako." Mheshimiwa
Mavunde alishauri.Mheshimiwa. Mavunde alihitimisha kwa kusisitiza
kwamba hizi pesa ambazo watu wanajishindia kupitia Tatumzuka ni fursa
hasa kwa vijana kujitengenezea ajira na kubadilisha maisha ya wale walio
karibu yao.
Afisa
wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bi Patty Mtatiro alielezea kwamba Tatu
Mzuka hadi sasa imetengeneza mamilionea 120 na kutoa zaidi ya shilingi
bilioni 5.3. Akasema kwamba sio hivyo tu, tarehe 19 Novemba ambapo ni
wiki mbili kutoka sasa Tatumzuka kupitia SUPA Mzuka Jackpot itatoa
milioni 150 za uhakika kwa mshindi atakayejishindia.
"
Kwa sasa unaweza kushinda kwa njia 3 kwa kucheza mara moja tu kwa
shilingi 500. Tatu Mzuka inakupa nafasi ya kushinda hadi Tz 6, 000,000
masaa 24 kwa siku. Kila Tzs500 unayoitumia inakupa nafasi ya moja kwa
moja kuingia kwenye Mzuka Jackpot ya kila wiki ambapo unaweza kushinda
zaidi ya shilingi Milioni 60. Namna ya tatu ni kupitia droo ya Supa
Mzuka Jackpot ambapo dau la uhakika la Milioni 150 litatolewa kwa
mshindi. Hakuna dili kali zaidi ya hili "alisema Bibi Mtatiro.
No comments :
Post a Comment