BENNY MWAIPAJA, DAR ES
SALAAM
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James
amewatoa hofu watanzania kuhusu ongezeko la Deni la Taifa akisisitiza kuwa Deni
hilo ni himilivu.
Bw. James amesema hayo Jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya
habari wakati wa hafla fupi ya kutia saini Mkataba wa mkopo wenye masharti
nafuu wa Shilingi bilioni 340 uliotolewa na... Benki ya Dunia kwa ajili ya Mradi
wa kuendeleza utalii kwa vivutio vilivyoko katika ukanda wa kusini mwa Tanzania
ujulikao kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW)
Alikuwa akitolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya watu na vyombo vya
habari vinavyozungumzia Deni la Taifa kwa kutumia neno Deni la Taifa “linapaa”
Katibu Mkuu huyo ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali
alisema kuwa Deni la Taifa ni himilivu kwa kutumia viwango vya kitaifa na
kimataifa kwamba ili nchi iwe katika hatari ya kukua kwa Deni lake la Taifa
inabidi lifikie asilimia zaidi ya 50 lakini kwa Tanzania kiwango cha deni hilo
ni asilimia 32.
“Deni letu lingekuwa linapaa, hata Benki ya Dunia wasingekubali
kutukopesha kwa maana hiyo tukitaka kukopa tutafanya hivyo kwa kuwa tuko chini
katika viwango vya ukopaji kwa asilimia zaidi ya 18” alisema Bw. Doto James.
Kwa hiyo nawaomba hili mlichukue muuelimishe umma wa watanzania
kwamba deni la Taifa ni stahimilivu, nchi inakopesheka vizuri.
Novemba 7, 2017, Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bungeni mjini Dodoma Mapendekezo ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maanndalizi ya Mpango na Bajeti kwa
Mwaka 2018/2019 alisema kuwa Deni la Taifa limefikia dola za Marekani milioni
26,115.2 mwezi Juni mwaka 2017.
Dkt. Mpango alieleza kuwa ongezeko hilo ni
sawa na asilimia 17 ikilinganishwa na dola milioni 22,320.76 katika kipindi
kama hicho mwaka 2016.
Alisema ongezeko hilo
lilichangiwa na mikopo mipya iliyochukuliwa ili kugharamia miradi ya maendeleo
kama vile: Standard Gauge Railway; Strategic Cities; mradi
wa usafirishaji Dar es Salaam (DART) na kupanua upatikanaji wa maji safi Dar es
Salaam.
No comments :
Post a Comment