Mratibu wa Kongamamo la Wasomi Wanataaluma wa Kikristo liitwalo Tanzania for Jesus Prayer Movement ambalo mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus, Ephrahim Mwambapa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Kanisa
la Abundant Bressing Center (ABC), Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam,
kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Hoteli ya Landmark siku ya
Jumamosi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli.
Mratibu wa Kongamano hilo, Ephrahim Mwambapa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.
Na Dotto Mwaibale
WANAFUNZI
waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kesho wanatarajia kufanya
kongamono kubwa la kihistoria kujadili namna... watakavyoweza kutumia
taaluma zao kusaidia jamii, kanisa na taifa kwa ujumla.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa Kongamamo hilo,
Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa
wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi
wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.
Alisema
licha ya muungano huo kuundwa na vijana wa kikristo lakini vijana wote
wasomi kutoka katika vyuo na shule za sekondari na madhehebu mbalimbali
wanaalikwa ili kuchangia mada zitakazo jadiliwa na mgeni rasmi atakuwa
ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu
Flaston Ndabila.
Mwambapa
alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali na
kuona ni jinsi gani kila mmoja na taaluma yake ataweza kusaidia jamii
badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kuifanyia kazi.
“Tunapokuwa
vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza
masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii
na ndio maana tumeona ni vizurio kuazisha muungano huu lengo likiwa
kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini” alisema
Mwambapa.
Alisema
wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano ya mkutano mkuu wa
kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na
kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mwambapa alisema kongamano hilo litahudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali,sekondari baadhi wa viongozi.
No comments :
Post a Comment