Mojawapo ya vifaa kwa ajili ya
mradi wa bwawa la samaki, pampu ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo
ikikabidhiwa kwa wanakikundi cha mradi huo kijiji cha Lubaga.
Wanakikundi na sehemu ya wananchi
wa kijiji hicho wakitayarisha bwawa tayari kwa ajili ya kusimikwa vifaa
na kuwekewa maji tayari kwa kuanza kupandikiza vifaranga vya samaki.
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi
Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki (katikati) akizungumza na
wananchi waliojitokeza katika zozezi hilo. Wengine pichani kushoto ni
Mwenyekiti wa kikundi hicho, Paula Kanuda na Afisa Ugani kutoka REDESO,
Erica Karutha.
Karatasi maalumu kwa ajili ya kutandaza bwawani kuzuia maji yasinyonywe na udongo likitolewa kwa kikundi hicho.
Diwani wa kata ya Kishapu, Mh.
Ali Shiganga akitoa neno la shukrani kwa mradi huo wakati wa mkabidhiano
ya vifaa vya bwawa la samaki kijiji cha Lubaga.
Mipira ya kuvutia maji kutoka kwenye chanzo na kuyaingiza bwawani ikikabidhiwa kwa wanakikundi cha mradi wa samaki.
Wananchi wakitandika karatasi maalumu kwa ajili ya kutandika kwenye bwawa kuzuia maji yasimezwe na udongo.
Mafundi wakifunga pampu kwa ajili ya kuvuta maji kitoka kwenye chanzo na kuyapeleka kwenye bwawa.
………………………………………………………………………………
Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Asasi isiyo ya kiserikali ya Msaada na Mandeleo ya Jamii (REDESO) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imetoa vifaa kwa ajili ya mradi wa bwawa la samaki kwa kikundi.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya sh.
milioni 4.3 vimetolewa kwa kikundi hicho kilichopo kijiji cha Lubaga
huku halmashauri hiyo ikiahidi kutoa sh. milioni 3 kwa ajili kununua
vifaranga vya samaki.
Katika makabidhiano hayo, vifaa
mbalimbali vikiwemo pampu ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo, wavu wa
kuweka juu ya bwawa kuzuia samaki kudhuriwa, mabomba ya kuvuta maji na
karatasi maalumu ya kutandika chini kuzuia maji yasinyonywe na udongo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo,
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce
Bagambabyaki aliishukuru REDESO na kuwataka wanakikundi hicho kuutunza
mradi kwani utakuwa na manufaa kwao na kijiji kizima.
Alisema mradi huo pia utatangaza
kijiji hicho kwa kuwa na kitoweo cha samaki kitakachokuwa kinapatikana
hapo na pia kutoa ajira hususan kwa mamalishe hivyo kujenga uchumi.
“Tumewaletea mradi huu hivyo ni
jukumu lenu kuutunza na mnatakiwa muweke uzio kuzuia mifugo isiingie
bwawani kunywa maji na kuwadhuru vifaranga wa samaki watakaopandwa,”
alisema Dk. Bagambabyaki.
Kwa upande wa Afisa Ugani kutoka
REDESO, Erica Karutha alisema lengo la mradi huo unaofadhiliwa na
Shirika la Irish Aid ni kuwakwamua kimaisha wanawake na vijana.
Karutha alisema kuwa wanaahidi
endapo mradi huo utafanya vizuri wataendelea kuwafadhili na hatimaye
uweze kuenea katika maeneo mengine ya wilaya hiyo.
Alisema shirika hilo linafanya
kazi kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji katika
halmashuri hiyo na kuwataka wananchi wengine wajitokeze kuchangamkia
fursa za miradi kama hiyo.
Kikundi hicho chenye jumla ya
wanachama 15 ambao wamejitolea kuchimba bwawa hilo kwa ajili ya
kupandikiza vifaranga vya samaki ambapo wamehukuru kwa msaada huo na
kuahidi kuutunza
No comments :
Post a Comment