Thursday, November 23, 2017

DR SHIKA AIBUKIA KWENYE MAHAFALI NA UZINDUZI WA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA KAHAMA,AAHIDI BILIONI 2




Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu leo amezidua rasmi chuo cha Sayansi ya afya kilichopo Mjini Kahama mkoani Shinyanga ambapo uzinduzi huo umeambatana na mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo hayo katika chuo hicho.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya wilaya ya Kahama akiwemo Mtanzania aliyejizolea umaarufu hivi karibuni Dr. Louis Shika ambaye ameahidi kutoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kusomesha wanachuo ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia ada na wale ambao ni yatima wazazi wao wamefariki dunia.



Akizungumza katika hahafali hayo yaliyofanyika leo Alhamis Novemba 23,2017 Nkurlu aliwataka wahitimu wa fani mbalimbali wilayani Kahama kuwa waadilifu pale wanapopata nafasi ya kuihudumia jamii ili kukidhi matakwa ya kusomea fani hizo.
Nkurulu alisema baadhi ya wahitimu wa mafunzo mbali mbali wamekuwa wakishindwa kukidhi vigezo kutokana na kutokuwa na nia ya dhati ya kutekeleza wajibu wao kwa weledi na uadilifu.
Katika hatua nyingine Nkurlu alimwelezea Dr. Shika kuwa ni mtu wa pekee mwenye utulivu na usikivu na kuongeza kuwa wadau wengine waige kama alichofanya Dr. Shika katika kuinua elimu nchini.
Kivutio kikuu katika sherehe hizo akawa Dr. Louis Shika ambaye hivi karibuni amejingea umaarufu, alipojitokeza katika mnada wa nyumba za kifahari za Bilionea Saidi Lugumi zilizoko jijini Dar es salaam, kupitia msemo wake wa “(900 INAPENDEZA)” ambapo katika mahafali hayo ameahidi kutoa bilioni mbili kila mwaka kusomesha watoto yatima katika wilaya ya Kahama.
Dr. Shika alisema kuwa yeye ni mpenzi wa elimu na anapenda watu wote wapate elimu hivyo kupitia kampuni yake ya Lancefort atasaidia kusomesha wanachuo ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia ada na wale ambao ni yatima wazazi wao wamefariki.
Ahadi hiyo imekuja kufuatia risala ya chuo hicho iliyosomwa na Mkuu wa Chuo hicho na kuelezea changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na wazazi kushindwa kulipa ada pamoja na waanachuo wengine kushindwa kuhitimu mafunzo yao baada ya wazazi wao kufariki.
Dr. Shika alitoa wito kwa ofisi ya mkuu wa wilaya imuombe kusaidia kusomesha wanafunzi wasio na uwezo kwani kampuni yake inauwezo wa kusaidia watoto yatima katika wilaya ya Kahama hivyo milango iko wazi na yeye yuko tayari kusaidia watu wenye njaa ya elimu.
Akielezea kiwango atakachokitoa kusomesha wanachuo hao, Dr Shika amesema kuwa itakuwa ni dola milioni moja za Kimarekani sawa na Bilioni mbili ambazo atakuwa anazitoa kila mwaka kwa chuo hicho kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wanaopenda kusoma lakini wanashindwa kutokana na ukosefu wa ada.
Katika hatua nyingine Dr Shika aliwataka waandishi wa habari na mwenye chuo wasimuulize kuhusu msaada huo ndani ya wiki mbili kwani kwasasa hana pesa bali wasubiri mpaka mchakato wake wa kuhamisha fedha zake kutoka Urusi ukamilike.
Naye mkurugenzi wa chuo hicho Yonah Bakungile amesema kuwa kumekuwa na shida ya wanafunzi wanaomaliza vyuo vya uuguzi kutokuwa na maadili na kufikilia masirahi jambo ambalo limechangia kupoteza maana halisi ya masomo hayo.
Aliwataka kuitumikia jamii bila kuangalia maslahi na kuwahudumia watu walio nacho na wasiokuwa nacho ikiwa ni kutimiza malengo na nia ya kuanzisha vyuo vya uuguzi katika kuihudumia jamii katika maeneo mbali hapa nchini.
Aidha alisema baadhi ya Wahitimu wa vyuo vya uuguzi wanakosa uadilifu na kuweka mbele maslahi binafsi hulka inayopoteza maana halisi ya fani hiyo.
Amewataka kuitumikia jamii bila ubaguzi na kuangalia maslahi binafsi ili kwenda sanjari na matakwa na viapo vya kada ya uuguzi duniani.
Katika Mahafali hayo ya kwanza, Jumla ya Wahitimu 33 wametunukiwa cheti cha Msingi katika Kozi ya Mwaka mmoja ya Ufamasia.
Chuo cha Sayansi ya Afya Kahama kilianzishwa mwaka 2016 kikitoa mafunzo katika fani za Ufamasia na Utabibu na kwamba jumla ya wanachuo 33 wamehitimu.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Wahitimu wakiingia ukumbini katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho.Picha zote kwa hisani ya Kijukuu blog
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiingia ukumbini kwa furaha wakiwa na furaha tele.
Wahitimu wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya akiwa na mkurugenzi wa Chuo hicho pamoja na mke wa mkurugenzi Mrs Bakungile.
Mwanachuo wa Chuo cha Sayansi ya Afya akionyesha burudani ya kucheza nyimbo za utamaduni wa Kisukuma katika mahafali hayo.
Mwanachuo akiendelea kutoa burudani katika uzinduzi wa chuo hicho.
Meza kuu ikifuatilia kwa makini burudani ya nyimbo za asili katika mahafali hayo.
Meza kuu ikifuatilia kwa makini burudani ya nyimbo za asili.
Familia na ndugu wa Mkurugenzi wa Chuo hicho wakiwa katika sherehe hizo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya Ndugu Yonah Bakungile akitoa neno kwa wahitimu katika mahafali hayo
Wageni waalikwa pamoja na wazazi wakiwa katika sherehe za mahafali na uzinduzi wa chuo cha sayansi ya afya
Mwenyekiti wa bodi ya shule akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Kahama kutoa hotuba yake.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akitoa hutuba kwa wazazi na wahitimu katika mahafali hayo.
Dr. Shika akitoa neno kwenye mahafali hayo
Dr. Shika akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu
Dr. Shika akishikana mkono na mkurugenzi wa chuo hicho
Mgeni muhimu wa katika mahafali hayo Dr. Louis Shika akipeana mkono na wageni wa meza kuu baada ya kutoa neno lake
Kikundi cha sanaa kutoka hospitali ya wilaya ya Kahama wakitoa burudani katika uzinduzi huo wa chuo
Burudani inaendelea
Wahitimu wakiwa wameketi katika nafasi zao
Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasubi Leonard Mayala kulia akiwa na Dr Louis Shika katika sherehe hizo
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akikakugua maabara ya kufundishia kwa vitendo katika Chuo hicho.
Mkuu wa wilaya ya Kahama akiendelea kupata maelekezo kuhusu elimu ya vitendo wanayoipata wanachuo katika chuo hicho.
Msafara wa mkuu wa wilaya ukikagua chumba cha Computer katika chuo hicho.
Elimu bora ni pamoja na mazingira bora ya kusomea na kufundishia,Hili ni moja ya darasa katika chuo cha Sayansi ya afya Kahama.
Masomo kwa vitendo,Hili ni moja ya darasa la kufundishia likiwa na vifaa vya kisasa vya kufundishia katika chuo hicho.
Masomo kwa Vitendo hiki ni chumba maalumu cha kufundishia kikiwa na mfano wa wodi ambapo wanafunzi wanafundishwa kwa vitendo namna ya kuhudumia wagonjwa wakiwa chuoni hapo.
Moja ya darasa la kufundishia katika chuo cha Sayansi ya afya kilichozinduliwa leo mjini Kahama.
Baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Kahama wakiwa katika sherehe hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama akiendelea kutembelea vyumba katika chuo hicho
Wanachuo wa mwaka wa kwanza na wa pili wakiwa katika mahafali hayo
Wazazi wakiwa katika mahafali hayo
Picha zote kwa hisani ya Kijukuu blog

No comments :

Post a Comment